515 Tafuta Ukweli ili Kutatua Matatizo Yako

1 Ukitaka kutia ukweli katika vitendo, na ukitaka kuuelewa, basi kwanza lazima uelewe kiini cha matatizo unayoyakabili na mambo yanayotokea karibu na wewe, na pia kipengele cha ukweli ambacho mambo haya yanahusiana nacho. Baada ya hapo, lazima utafute ukweli kulingana na matatizo yako halisi. Kwa njia hiyo, unapokuwa ukipata uzoefu polepole, utaweza kuuona mkono wa Mungu katika kila kitu kinachokutendekea, na vile vile kile Anachotaka kufanya na matokeo Anayotaka kutimiza ndani yako.

2 Ukijipima tu dhidi ya ukweli wa neno la Mungu wakati unapokuwa ukila na kunywa neno la Mungu kwenye mikusanyiko, au unapokuwa ukitekeleza wajibu wako, na ikiwa unahisi kuwa vitu ambavyo kwa kawaida hufanyika katika maisha yako havihusiani na imani yako au ukweli, na ukihisi kuwa unaweza kuvishughulikia na kisha ufanye hivyo kwa kutegemea falsafa yako ya maisha, basi hutapata ukweli kamwe, na kamwe hutaelewa kile ambacho Mungu anataka kutimiza ndani yako au matokeo Anayotaka kupata.

3 Kufuatilia ukweli ni mchakato mrefu. Kuna upande rahisi, na pia kuna upande mgumu. Kwa ufupi, tunapaswa kutafuta ukweli na kutenda na kupitia neno la Mungu katika kila kitu kinachotokea karibu nasi; mara unapoanza kufanya hivi, utaona zaidi na zaidi kiasi cha ukweli ambacho unapaswa kupata na kufuatilia katika imani yako katika Mungu, na kwamba ukweli ni halisi kabisa na ukweli ni uzima.

Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kufuatilia Ukweli na Njia ya Kuufuatilia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 514 Njia ya Kutafuta Ukweli

Inayofuata: 516 Kubali Neno la Mungu ili Uwe na Uzoefu wa Kina

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp