843 Wewe ni Mtu Anayetafuta Kukamilishwa na Mungu?

1 Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: “Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema; ni hukumu Yake na adabu ambazo zimenilinda na kunitakasa.

2 Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu.

3 Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa.” Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Wanapokuwa na uzoefu mpaka mwisho kabisa, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika wataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 842 Unapaswa Kutafuta Kukamilishwa na Mungu Katika Vitu Vyote

Inayofuata: 844 Mungu Atakukamilisha Ukiitembea Tu Njia ya Petro

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp