644 Kutumika kama Foili ni Baraka ya Milele
1 Ni kwa sababu ninyi mnaishi katika ulimwengu uleule, nchi hiyo hiyo chafu, sawa na Mungu, kwamba ninyi ni foili na mnapokea wokovu mkubwa zaidi. Mungu asingekuwa mwili, ni nani angekuwa na huruma kwenu, na ni nani angewatunza, watu duni kama ninyi? Nani angewajali? Mungu asingekuwa mwili ili Afanye kazi miongoni mwenu, mngepokea lini wokovu huu ambao wale waliokuwa kabla yenu hawakuwahi kuupata? Nisingekuwa mwili ili Niwajali, Nihukumu dhambi zenu, je, si mngelikuwa mmeanguka kuzimu kitambo?
2 Nisingekuwa mwili na kujinyenyekeza miongoni mwenu, mngewezaje kustahili kuwa foili kwa tabia ya Mungu yenye haki? Je, ninyi si foili kwa sababu Nilichukua umbo la binadamu na kuja miongoni mwenu ili kuwawezesha kupata wokovu mkubwa zaidi? Je, hampokei wokovu huu kwa sababu Nimekuwa mwili? Mungu asingekuwa mwili ili Aishi nanyi, je, bado mngegundua kuwa mnaishi maisha ya mateso hapa duniani, ambayo ni mabaya kuliko mbwa na nguruwe? Je, hamjaadibiwa na kuhukumiwa kwa sababu ninyi ni foili kwa kazi Yangu katika mwili?
3 Hakuna kazi inayofaa zaidi kwenu kuliko kazi ya foili, kwa kuwa ni kwa sababu ninyi ni foili ndiyo mnaokolewa katikati ya hukumu. Je, hamhisi kuwa kustahilishwa kutenda kama foili ni baraka yenu kubwa zaidi ya maisha? Ninyi hufanya kazi ya foili tu, lakini mnapokea wokovu kiasi ambacho hamjawahi kuwa nacho au hata kufikiria. Leo, jukumu lenu ni kuwa foili, na thawabu yenu ya haki ni kupokea baraka za milele katika siku za baadaye. Wokovu mnaoupata si ufahamu wa muda mfupi au ufahamu fulani wa muda kwa ajili ya wakati huu, lakini baraka kubwa zaidi: mwendelezo wa milele wa maisha.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa” katika Neno Laonekana katika Mwili