618 Hudumu Jinsi walivyofanya Waisraeli
1 Matakwa mnayohitaji kutimiza leo—kufanya kazi pamoja kwa upatanifu—ni sawa na huduma ambayo Yehova alitaka kutoka kwa Waisraeli: Vinginevyo, acheni tu kufanya huduma. Kwa sababu ninyi ni watu wanaomhudumia Mungu moja kwa moja, angalau lazima muweze kuwa waaminifu na watiifu katika huduma yenu, na pia lazima muweze kupata mafunzo kwa njia ya utendaji. Kwa wale kati yenu wanaofanya kazi kanisani hasa, je, kuna yeyote kati ya akina ndugu walio chini yenu anayeweza kuthubutu kuwashughulikia? Je, mtu yeyote anaweza kuthubutu kuwaambia makosa yenu ana kwa ana? Mko juu ya wengine wote, mnatawala kama wafalme! Hata hamchunguzi ama kuingia katika mafunzo ya utendaji ya aina hii, lakini bado mnazungumza kuhusu kumhudumia Mungu!
2 Kwa sasa, unaombwa uyaongoze makanisa kadhaa, lakini hukosi tu kujitolea, bali hata unashikilia mawazo na maoni yako mwenyewe. Kamwe huwajibikii mambo mengi ambayo yanapaswa kushughulikiwa, ama unaridhika tu, kila mmoja wenu akijadili maoni yake mwenyewe na kuilinda hadhi, sifa na heshima yake mwenyewe kwa uangalifu. Hakuna yeyote kati yenu aliye tayari kujinyenyekeza, na hakuna atakayechukua hatua ya kwanza kujitolea na kufidiana kasoro zenu ili maisha yasonge mbele upesi zaidi. Wakati wowote mnapokabiliwa na chochote, mnapaswa kufanya ushirika ninyi kwa ninyi ili maisha yenu yaweze kufaidika. Baada ya kutembelea makanisa yote, mnapaswa kukusanyika pamoja na kushiriki kuhusu masuala yote mnayogundua na matatizo yoyote mliyokumbana nayo katika kazi yenu, na kisha mnapaswa kuwasiliana kuhusu nuru na mwangaza ambao mmepokea—huu ni utendaji wa msingi wa huduma.
3 Lazima mfanikishe ushirikiano wa upatanifu kwa ajili ya kazi ya Mungu, kwa manufaa ya kanisa, na ili muwahimize ndugu zenu mbele. Mnapaswa kushirikiana, kila mmoja akimrekebisha mwenzake na kufikia matokeo bora ya kazi, ili kuyatunza mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo maana ya ushirikiano wa kweli, na ni wale tu wanaoshiriki katika ushirikiano huo ndio watakaopata kuingia kwa kweli. Kama watu wanaomhudumia Mungu, kila mmoja wenu lazima aweze kulinda maslahi ya kanisa katika kila kitu mnachofanya, badala ya kuzingatia tu masilahi yenu wenyewe. Haikubaliki ninyi kutenda kila mtu peke yake, daima mkidhoofishana. Watu wanaotenda kwa namna hiyo hawafai kumhudumia Mungu! Watu kama hao wana tabia mbaya sana; hawana ubinadamu hata kidogo ndani yao. Wao ni Shetani asilimia mia moja! Wao ni wanyama!
Umetoholewa kutoka katika “Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu” katika Neno Laonekana katika Mwili