608 Jinsi ya Kuhudumu Kwa Uuwiano na Mapenzi ya Mungu

1 Ikiwa ungependa kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanamfurahisha Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza unafaa kuingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu.

2 Na unapomhudumia ndipo Mungu hufungua macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zako, ili muweze kutumia nguvu za kila mmoja kufidia upungufu wako na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zenu. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 607 Kiwango cha Chini Zaidi cha Kuwa Mtu Anayemtumikia Mungu

Inayofuata: 609 Ni Wandani wa Mungu Pekee Wanaostahili Kumtumikia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp