25 Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi

Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinazipindua mbingu na dunia, na zinaenea kote angani!

1 Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha kutoka kwayo. Nuru za umeme na ngurumo zinatolewa, mbingu na nchi zinabadilishwa mara moja, na watu wako karibu kufa. Kisha, dhoruba kali sana ya mvua inaufagilia mbali ulimwengu wote kwa haraka sana, ikinyesha kutoka angani! Kama kiasi kidogo chenye baridi cha nuru za umeme, ngurumo zinawafanya watu kutetemeka kwa hofu! Upanga mkali wa kukata kuwili unawaangamiza wana wa uasi, sauti za kuomboleza zinatokea ghafla. Wengine wanaamka kutoka katika usingizi wao, na, wakiwa wameshtuka sana, wao wanachunguza nafsi zao na kukimbia mara moja mbele ya kiti cha enzi. Wanakoma kufanya hila na kudanganya na kufanya uhalifu, nami Sijachelewa sana kuwaamsha watu kama hao.

2 Naangalia kutoka katika kiti cha enzi. Natazama ndani ya mioyo ya watu. Nawaokoa wale ambao wanitamani sana kwa dhati na kwa ari, nami Ninawahurumia. Nitawaokoa milele wale wanaonipenda mioyoni mwao zaidi ya vingine vyote, wale wanaoyaelewa mapenzi Yangu, na ambao wananifuata hadi mwisho. Kutoka wakati huu na kuendelea, hukumu ya kiti cha enzi cheupe kikuu imefunuliwa waziwazi kwa raia na imetangazwa kwa watu wote kuwa hukumu imeanza! Bila shaka, wote ambao hawaneni yaliyo mioyoni mwao, wale wanaohisi kuwa na wasiwasi na hawathubutu kuwa na hakika, wale ambao hupoteza wakati, ambao wanayaelewa mapenzi Yangu lakini hawako radhi kuyatenda, sharti wahukumiwe. Kutoka katika kiti cha enzi hadi ulimwengu na miisho ya dunia, ngurumo saba zinasikika. Kikundi kikubwa cha watu kitaokolewa na kutii mbele ya kiti Changu cha enzi.

3 Baada ya huu mwanga wa uzima, watu wanatafuta njia ya kuishi nao hawana budi kuja Kwangu, kupiga magoti katika ibada, midomo yao inaliita jina la Mwenyezi Mungu wa kweli. Acha wale walio katika miisho ya dunia waone kwamba Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ni upendo, Mimi ni huruma, Mimi ni uadhama, Mimi ni moto wenye ghadhabu, na hatimaye Mimi ni hukumu isiyo na huruma. Watu wote wanaamini kabisa na hakuna mtu anayethubutu kunipinga tena, kunihukumu au kunikashifu tena. wacha ijulikane katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia, katika kila nyumba na kwa watu wote: Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli. Mataifa na watu wote watatii mbele Yangu milele yote!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 35” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 24 Anayeachilia Ngurumo Saba

Inayofuata: 26 Matarumbeta Saba ya Mungu Yanasikika Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp