26 Matarumbeta Saba ya Mungu Yanasikika Tena

1 Matarumbeta Yangu saba yatapaza sauti, kuamsha walio lala! Shughulika kwa haraka, muda hujakwisha. Angalia maisha yako! Fungua macho yako na uone ni wakati upi sasa. Ni nini unatafuta? Kuna nini ya kufikiri? Na ni nini kilicho cha kushikilia? Je, inawezekana kuwa bado hujafikiria tofauti katika thamani kati ya kupata maisha Yangu na mambo yote unayopenda na kushikilia? Acha kuwa makaidi na kucheza kila mahali. Usikose nafasi hii. Wakati huu hautakuja tena! Simama mara moja, tenda kufanyisha roho yako mazoezi, kutumia zana mbalimbali kukuwezesha na kuzuia kila njama na hila za Shetani, na umshinde Shetani, ili kwamba uzeofu wako wa maisha uweze kuwa wa kina zaidi na uweze kuishi kwa kudhihirisha tabia Yangu, ili maisha yako yaweze kukomaa na yawe yenye tajriba na ili uweze daima kufuata nyayo Zangu. Ukiwa bila hofu, ukiwa usiye udhaifu, daima ukisonga mbele, hatua kwa hatua, moja kwa moja hadi mwisho wa njia!

2 Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti tena, itakuwa mwito wa hukumu, hukumu ya wana wa uasi, hukumu ya mataifa yote na watu wote, na kila taifa litajisalimisha mbele ya Mungu. Uso wa utukufu wa Mungu hakika utaonyeshwa mbele ya mataifa yote na watu wote. Kila mtu atakuwa ameridhishwa kabisa, kupiga kelele kwa Mungu wa kweli bila kikomo. Mwenyezi Mungu Atakuwa Mtukufu zaidi, na wanangu watashiriki katika utukufu, kushiriki ufalme nami, kuhukumu mataifa yote na watu wote, kuadhibu maovu, kuokoa na kuwa na huruma juu ya watu ambao ni Wangu, kuleta uthabiti na utulivu kwa ufalme. Kupitia sauti ya matarumbeta saba, kundi kubwa la watu litaokolewa, kurudi mbele Yangu kupiga magoti na kuabudu, kwa sifa daima!

3 Wakati matarumbeta saba zitatoa sauti mara nyingine tena, hilo litakuwa tukio la hitimisho la mwisho wa enzi, mlipuko wa sauti wa tarumbeta ya ushindi dhidi ya ibilisi Shetani, saluti katika mwanzo wa maisha ya wazi wa ufalme duniani! Sauti hii ya kifahari sana, sauti hii inayonguruma pande zote za kiti cha enzi, mlipuko wa sauti ya tarumbeta inayotikisa mbingu na dunia, ni ishara ya mpango Wangu wa usimamizi, na hukumu ya Shetani, kuadhibu duniani hii ya zamani kwa kifo kabisa, jahanamu! Huu mlipuko wa sauti ya tarumbeta unaashiria kwamba lango la neema ni linafungika, kwamba uhai wa ufalme utaanza duniani, ambayo ni kamilifu kabisa. Mungu Huokoa wale wanaompenda. Mara tu watakaporudi kwa ufalme Wake, watu duniani watakabili njaa, ndwele ya kufisha, na mabakuli saba ya Mungu, tauni saba zitaanza kutumika kwa mfululizo. Mbingu na dunia zitapita, lakini neno Langu halitapita!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 36” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 25 Ngurumo saba zinatoka katika kiti cha enzi

Inayofuata: 27 Umeme Uwakapo Kutoka Mashariki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp