Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Binadamu na Mungu Washiriki katika Furaha Kamili ya Muungano

I

Mungu ameanza kazi Yake kote ulimwenguni.

Watu huko wazinduka na kuizunguka kazi Yake kote.

Wakati Mungu "anasafiri" ndani yao, wao wavunja vifungo vya Shetani.

Kutoka kwa vifungo vya mateso makubwa, sasa wako huru milele.

Siku ya Mungu inapofika, watu wote wanafurahi.

Huzuni mioyoni mwao sasa imetoweka milele.

Mawingu ya simanzi yanatoweka, upepo mwanana unaelea bila vikwazo.

Mungu anafurahia furaha ya umoja na mwanadamu.

Watu wote wanapomsifu Mungu, Anatukuzwa katika vitu vyote.

Anga inageuka bluu ng'avu. Maua yanachanua, majani yanakuwa ya kijani zaidi.

Vitu vyote duniani vinakuwa vizuri sana.

II

Vitendo vya mwanadamu vinampa Mungu cha kufurahia, na hivyo Mungu haudhiki tena.

Na, vikiambatana na ufikaji wa siku ya Mungu, vitu vyenye uzima duniani vinapata tena kiini cha kuweko kwavyo,

vitu vyote duniani vinachangamka tena, na kumchukua Mungu kama msingi wa kuweko kwavyo,

kwa kuwa Anavifanya vitu vyote ving'ae na maisha, na hivyo, pia, Anavifanya vitoweke kimya kimya.

Vitu vyote vinasubiri neno la Mungu linalozungumzwa na kinywa Chake.

Na wote wanafurahia kile Anachosema na kufanya.

Yeye ndiye Aliye Juu, lakini pia huishi na mwanadamu.

Matendo yao, yanadihirisha uumbaji wa Mungu wa dunia na mbinguni juu.

Watu wote wanapomsifu Mungu, Anatukuzwa katika vitu vyote.

Anga inageuka bluu ng'avu. Maua yanachanua, majani yanakuwa ya kijani zaidi.

Vitu vyote duniani vinakuwa vizuri sana.

III

Kwa sauti Yake, mtu anaenda huku na huko.

Watu katika ufalme Wake wamejaa furaha; maisha yao yanakua.

Mungu anafanya kazi kati ya wateule.

Kazi Yake haiwezi kutiwa doa na fikira za wanadamu.

Kwa maana Mungu anafanya kazi Yake mwenyewe.

Mungu anapofanya kazi Yake, kila kitu chafanywa upya na kubadilishwa.

Wakati kazi ya Mungu imekamilika,

mtu anarejeshwa, hakuna tena kudhikishwa na kile Mungu anauliza.

Nchi inabarikiwa na furaha!

Watu wote wanapomsifu Mungu, Anatukuzwa katika vitu vyote.

Anga inageuka bluu ng'avu. Maua yanachanua, majani yanakuwa ya kijani zaidi.

Vitu vyote duniani vinakuwa vizuri sana.

Nchi itakapojaa furaha,

Mungu atachukua fursa hii kuwabariki wanadamu wote.

kutoka katika "Tamko la Thelathini na Tatu" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Ukweli wa Matokeo ya Kupotoshwa kwa Mwanadamu na Shetani

Inayofuata:Unapaswa Kuyachukuliaje Maneno na Vitendo Vyako Mwenyewe

Maudhui Yanayohusiana