933 Mwanadamu Anapaswa Kuthamini Viumbe wa Mungu
Hivyo ni aina gani ya mtazamo ambao mwanadamu anapaswa kuwa nao kwa vitu vyote? Vithamini sana, vitunze, vitumie kwa ufanisi.
1 Mungu anamwacha mwanadamu kusimamia vitu vyote na kuwa na utawala juu yao, lakini mwanadamu anafanya kazi nzuri? Mwanadamu ana tabia ya uharibifu; mwanadamu sio kwamba tu hawezi kutunza vitu kama Mungu alivyoviumba, kwa kweli ameviharibu. Binadamu ameifanya milima kuwa vifusi, ameijaza bahari kwa mchanga, na amezibadilisha tambarare kuwa majangwa ambapo hakuna kinachoweza kuishi. Halafu katika majangwa hayo mwanadamu amejenga viwanda na kujenga vinu vya nyuklia na uharibifu unaendelea katika pande zote. Mito si mito tena, bahari si bahari tena….
2 Binadamu anapovunja uwiano na kanuni za maumbile, siku yao ya maafa na kifo haipo mbali na haiepukiki. Maafa yanapokuja, watajua viumbe vya Mungu ni vya thamani kiasi gani jinsi vyote ni muhimu kwa binadamu. Mwanadamu kuishi katika mazingira yenye hali ya hewa nzuri ni sawa na kuwa peponi. Watu hawatambui baraka hii, lakini wakati ambapo wataipoteza yote ndipo watatambua ni jinsi gani yote ni adimu na ya thamani.
3 Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuirudisha hii yote? Ikiwa Mungu hafanyi chochote, ikiwa Mungu hatamani tena kufanya kitu chochote kwa ajili ya binadamu—yaani, hataki kuingilia—njia bora zaidi ingekuwa ni binadamu kusitisha uharibifu huu na kurudisha vitu kuwa vile vilivyokuwa. Kusitisha uharibifu huu wote humaanisha kusitisha uporaji na uharibifu wa vitu ambavyo Mungu ameviumba. Hii itaruhusu mazingira ambamo mwanadamu anaishi kuboreka taratibu. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha uharibifu zaidi wa mazingira na hali itakuwa mbaya zaidi.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” katika Neno Laonekana katika Mwili