737 Mwanadamu Anapaswa Kuwa na Moyo Umwogopao Mungu
1 Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au mijibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu.
2 Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
3 Kama unaweza kutimiza hoja hii kati ya zote, na kumiliki mwelekeo huu kati ya yote, basi Mungu hatakulaumu wewe kwa upumbavu wako, kutojua kwako, na ukosefu wa kuelewa kwa sababu zinazosababisha vitu. Badala yake, kutokana na hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa nia za Mungu, na mwelekeo wako wa kuwa radhi kumtii Yeye, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukuangaza wewe, au kustahimili kutokuwa mkomavu kwako na kutojua kwako. Kinyume chake, endapo mwelekeo wako kwake Yeye utakuwa usioheshimu—kuhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua maana ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa taarifa. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako.
4 Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine: Unapaswa uwe makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Kama unaweza kwa kweli kutenda haya kulingana na kanuni hizi kila pahali, katika hali zote, katika vitu vyoye, nyakati zote, na kushikilia mtazamo wa aina hiyo hasa wakati huelewi kitu basi Mungu siku zote atakuongoza wewe, na kukupa na hata njia ya kufuata.
Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha” katika Neno Laonekana katika Mwili