555 Unapaswa Kufuatilia Maendeleo Mema
Natumaini kwamba watu wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu, kuwa wanaweza kuwa wenye mawazo sawa katika kumridhisha Mungu kwa ajili ya maadili ya pamoja, na wanaweza kuendelea pamoja katika njia ya kuelekea kwa ufalme. Kuna haja gani ya kuja na dhana zisizohitajika? Ni kuweko kwa nani kufikia leo hakujakuwa kwa ajili ya Mungu? Na kwa kuwa ni hivyo, kuna haja gani ya huzuni, ghamu, na tanafusi? Hili halina faida kwa mtu yeyote. Maisha yote ya watu yapo mikononi mwa Mungu, na isingekuwa kwa ajili ya azimio lao mbele ya Mungu, ni nani angekuwa radhi kuishi bure katika dunia hii tupu ya mwanadamu? Kwa nini ujisumbue? Kurupuka ndani na nje ya ulimwengu, wasipomfanyia Mungu chochote, je, maisha yao yote hayatakuwa ya bure? Hata kama Mungu hayaoni kwamba matendo yako yanastahili kutajwa, je, hutatoa tabasamu la kuridhika wakati wa kifo chako? Unapaswa kufuatilia maendeleo ya kujenga, sio kurudi nyuma hasi—je, huu sio utendaji bora?
Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 39” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili