398 Unapaswa Kutafuta Kumpenda Mungu Katika Imani Yako

1 Mtu anayemtumikia Mungu lazima asijue jinsi ya kuteseka kwa ajili Yake; zaidi ya hayo, anapaswa kuelewa kwamba kusudi la kuamini katika Mungu ni kwa ajili ya kufuatilia kumpenda Mungu. Mungu hukutumia si kwa sababu tu ya kukusafisha au kwa sababu ya kukufanya uteseke, lakini badala yake ni Yeye hukutumia ili uweze kujua matendo Yake, kujua umuhimu halisi wa maisha ya binadamu, na hasa, ili uweze kujua kwamba kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Kupata uzoefu wa kazi ya Mungu hakuhusu kufurahia neema Yake, bali kuhusu kuteseka kwa sababu ya upendo wako Kwake. Kwa kuwa unafurahia neema ya Mungu, lazima pia ufurahie kuadibu Kwake; lazima upitie haya yote. Unaweza kupata uzoefu wa nuru ya Mungu ndani yako, na unaweza pia kupitia jinsi Anavyokushughulikia na Anavyokuhukumu. Kwa njia hii, uzoefu wako utakuwa mkamilifu.

2 Mungu ametekeleza kazi Yake ya hukumu na kuadibu kwako. Neno la Mungu limekushughulikia, lakini si hilo yu; pia limekupa nuru, na kukuangazia. Wakati wewe ni hasi na dhaifu, Mungu ana wasiwasi kwa ajili yako. Hizi kazi zote ni za kukufahamisha kwamba kila kitu kuhusu mwanadamu kimo katika udhibiti wa Mungu. Unaweza kufikiri kwamba kuamini katika Mungu ni kuhusu mateso, au kumfanyia mambo ya kila aina; unaweza kufikiri kwamba sababu ya kumwamini Mungu ni ili mwili wako uwe na amani, au ili kwamba kila kitu maishani mwako kiende vizuri, au ili kwamba uweze kuwa na raha na utulivu katika kila kitu. Hata hivyo, hakuna kati ya haya ambayo watu wanapaswa kuhusisha na imani yao katika Mungu. Ukiamini kwa ajili ya sababu hizi, basi mtazamo wako si sahihi na haiwezekani kabisa wewe kukamilishwa.

3 Matendo ya Mungu, tabia ya Mungu ya haki, hekima Yake, maneno Yake, na maajabu Yake na kutoeleweka kwa kina Kwake yote ni mambo ambayo watu wanapaswa kuelewa. Kuwa na ufahamu huu, unapaswa kuutumia kuondoa moyoni mwako madai, matumaini na fikiza za kibinafsi. Ni kwa kuondoa mambo haya tu ndiyo unaweza kukidhi masharti yanayotakiwa na Mungu, na ni kwa kufanua hivi tu ndiyo unaweza kuwa na uzima na kumridhisha Mungu. Kusudi la kumwamini Mungu ni ili kumridhisha na kuishi kwa kudhihirisha tabia ambayo Yeye anahitaji, ili matendo na utukufu Wake viweze kudhihirishwa kupitia kundi hili la watu wasiostahili. Huu ndio mtazamo sahihi wa kuamini katika Mungu, na hili pia ndilo lengo unalopaswa kutafuta.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 397 Kumwamini Mungu ni Kutafuta Kumjua Mungu

Inayofuata: 399 Njia ya Kumwaamini Mungu Ndiyo Njia ya Kumpenda

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp