262 Umesikia Mwenyezi Akitanafusi?

1 Alfajiri inapofika, nyota ya asubuhi inaanza kuangaza mashariki. Hii ni nyota ambayo haijawahi kuwepo hapo awali. Inaliangaza anga lililo bado na nyota, ikikuwasha nuru iliyozimwa katika mioyo ya wanadamu. Binadamu si wapweke tena, kwa sababu ya mwanga huu, ambao hukuangazia wewe sawia na wengine. Lakini ni wewe tu unayebaki ukiwa umelala fofofo katika usiku wa giza. Huwezi kuisikia sauti, wala kuiona nuru, hujui kuhusu ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, enzi mpya, kwa sababu baba yako hukwambia, “Mwanangu, usiamke, bado ni mapema. Hali ya anga ni baridi, kwa hivyo usiende nje, usije ukachomwa machoni kwa mkuki na upanga.” Unaamini maonyo ya baba yako pekee, maana unaamini kwamba baba yako tu ndiye yuko sahihi, kwa sababu baba yako ana umri mkubwa kuliko wewe na kwamba baba yako anakupenda sana.

2 Maonyo kama hayo na upendo kama huo unakufanya uwache kuamini hekaya kwamba kuna nuru ulimwenguni, na uwache kujali kama ukweli bado upo ulimwenguni humu. Huthubutu tena kutumainia ukombozi kutoka kwa mwenye Uweza. Umeridhika kuwa katika hali hiyo, hutumainii tena ujio wa nuru, na hutazamii tena kuja kwa Mwenye uweza kama ilivyo katika hekaya. Inavyokuhusu wewe, yote yaliyo mazuri hayawezi kufufuliwa tena, wala hayawezi kuendelea kuwepo. Kesho ya wanadamu, siku za baadaye za wanadamu zinapotea, zinaharibika kabisa machoni pako. Unayashika sana mavazi ya baba yako kwa nguvu zako zote, ukifurahia kushiriki taabu zake, ukihofu sana kumpoteza mwenzako wa kusafiri na mwelekeo wa safari yako ya mbali. Ulimwengu huu mkubwa na wenye giza wa binadamu umewaunda wengi wenu, kuwa majasiri na watu wa kujitahidi sana katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ulimwengu huu. Umewaunda “mashujaa” wengi ambao hawaogopi kifo kabisa. Zaidi ya hayo, umetengeneza kundi baada ya kundi la watu waliokufa ganzi na wanadamu waliopooza ambao hawajui makusudi ya kuumbwa kwao.

3 Macho ya Mwenye uweza hukagua kila mmoja wa jamii ya wanadamu walio katika mateso makali. Anachosikia ni vilio vya wale wanaoteseka, Anachoona ni kutokua kwa aibu kwa wale wanaoteseka, na Anachohisi ni kutojiweza na hofu ya jamii ya wanadamu ambayo imepoteza neema ya wokovu. Wanadamu wanakataa utunzaji Wake, wakichagua kutembea katika njia yao wenyewe, na wakijaribu kukwepa macho Yake yanayochunguza kwa karibu, wakiona ni afadhali waonje uchungu wa kilindi cha bahari hadi mwisho, pamoja na adui. Kutanafusi kwa Mwenye uweza hakusikiki tena na binadamu. Mikono ya Mwenye uweza haiko tayari kuwapapasa tena wanadamu hawa wenye huzuni. Anarudia kazi Yake, mara kwa mara akikamata tena, na mara kwa mara akipoteza tena, na kutoka wakati huo, Yeye anaanza kuchoka, kujihisi mchovu, na hivyo Anasitisha kazi inayofanyika, na kuwacha kutembea kati ya wanadamu…. Wanadamu hawana ufahamu kabisa kuhusu mabadiliko haya, hawajui kuhusu kuja na kuondoka, huzuni na ghamu ya Mwenye uweza.

Umetoholewa kutoka katika “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 261 Mungu Asikitikia Mustakabali wa Binadamu

Inayofuata: 263 Siri Moyoni Mwako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Tafadhali weka neno unalotafuta katika kisanduku cha kutafuta

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp
Yaliyomo
Mipangilio
Vitabu
Tafuta
Video