198 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu Mara Mbili
1 Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.
2 Mungu Anapokuwa mwili tu ndipo Atakapoishi pamoja na mwanadamu, kuzoea mateso ya dunia, na kuishi katika mwili wa kawaida. Ni kwa namna hii tu ndipo Ataweza kuwapa wanadamu njia ya vitendo wanayohitaji kama viumbe. Mwanadamu anapokea wokovu kamili kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sio moja kwa moja kutoka kwa maombi yao kwenda mbinguni. Kwani mwanadamu ni mwenye mwili; mwanadamu hawezi kuona Roho wa Mungu na pia kutoweza kumkaribia. Kile tu mwanadamu anaweza kushiriki ni mwili wa Mungu; kupitia Yeye tu ndipo mwanadamu ataweza kuelewa njia zote, na ukweli wote, na kupokea wokovu kamili.
3 Kupatikana kwa mwili mara ya pili kunatosha kumaliza dhambi za mwanadamu na kumtakasa mwanadamu. Hivyo, kupatikana kwa mwili mara ya pili kutafikisha tamati kazi yote ya Mungu mwenye mwili na kukamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili. Baada ya hapo, kazi ya Mungu mwenye mwili itakuwa imefika mwisho kabisa. Baada ya kupata mwili mara ya pili, hatakuwa mwili tena kwa kazi Yake. Kwani usimamizi Wake wote utakuwa umefika mwisho. Katika siku za mwisho, mwili Wake utakuwa umepata watu Wake teule kabisa, na yote mwanadamu katika siku za mwisho watakuwa wameainishwa kulingana na aina. Hatafanya kazi ya wokovu tena, wala Hatarudi kuwa mwili ili kutekeleza kazi yoyote.
Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili