401 Umuhimu wa Kumwamini Mungu ni Mkubwa Sana

1 Haijalishi ni kwa muda gani mmemwamini Mungu, bado hamjapata ufahamu kamili wa umuhimu wa imani kwa Mungu. Kwa hakika, umuhimu wa imani kwa Mungu ni mkubwa kiasi kwamba watu hawawezi kuuelewa. Mwishowe, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo ni ya Shetani na mambo ya asili yao lazima yabadilike na lazima yalingane na mahitaji ya ukweli; ni kwa njia hii tu ndiyo mtu anaweza kupata wokovu kwa kweli. Iwapo, kama ulivyofanya wakati ulikuwa ndani ya dini, unatoa tu baadhi ya maneno ya mafundisho au kupiga kelele ukitaja kaulimbiu, na kisha utende vitendo vichache vizuri, uonyeshe tabia nzuri zaidi na kuepuka kutenda dhambi kiasi, dhambi zozote za waziwazi, hii bado haimaanishi kwamba umeingia katika njia sahihi ya kumsadiki Mungu.

2 Je, kuweza kuzitii sheria kunaonyesha kwamba unaitembelea njia sahihi? Kama mambo ndani ya asili yako hayajabadilika, na mwishowe ungali unampinga na kumkosea Mungu, basi hili ndilo tatizo lako kubwa zaidi. Iwapo, katika imani yako kwa Mungu, hulitatui tatizo hili, basi unaweza kuchukuliwa kuwa aliyeokolewa? Namaanisha nini kwa kusema hili? Nataka kuwafanya nyote muelewa ndani ya mioyo yenu kwamba imani kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu, na Mungu au na ukweli. Lazima uichague njia yako vyema, utie jitihada katika ukweli, na kutia jitihada ndani ya maneno ya Mungu. Usipate tu maarifa kiasi ya kijinga au kupata ufahamu kadiri, na kisha kufikiri kuwa umemaliza; ukijidanganya, utajidhuru tu mwenyewe.

3 Watu hawafai kupotoka katika imani yao kwa Mungu; mwishowe, ikiwa hawana Mungu ndani ya mioyo yao, na wanashikilia tu kitabu na kukiangalia kwa muda mfupi tu, na wasiwache nafasi ya Mungu ndani ya mioyo yao, basi wameangamia. Ni nini maana ya maneno haya, “Imani ya binadamu kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu”? Je, yanapinga maneno, “Imani katika Mungu haiwezi kutenganishwa na Mungu”? Unawezaje kuwa na Mungu ndani ya moyo wako kama maneno ya Mungu hayamo ndani ya moyo wako? Kama unamsadiki Mungu, lakini moyo wako hauna Mungu wala maneno Yake, wala uongozi Wake, basi umeangamia kabisa. Kama huwezi kufanya jambo dogo kulingana na hitaji la Mungu, basi ukikumbana na suala kubwa la kanuni utakuwa hata na uwezo mdogo zaidi kulitimiza hitaji la Mungu. Hii inamaanisha huna ushuhuda.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 400 Ufuatiliaji Unaopaswa Kufuatwa na Waumini

Inayofuata: 402 Ni Wale tu Wenye Imani ya Kweli Ndio Wanapata Idhini ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp