661 Wafuasi wa Kweli wa Mungu Wanaweza Kusimama Imara Katika Majaribio
1 Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho. Wale ambao wamekabiliwa na taabu ni wale wasiokuwa na kazi ya Roho Mtakatifu na uelekezi wa Mungu, lakini wale ambao wameshindwa kwa kweli na wanatafuta mapenzi ya Mungu kwa kweli hatimaye watasimama imara; ndio wale ambao wana ubinadamu, na wanaompenda Mungu kwa kweli. Bila kujali Mungu hufanya nini, hawa washindi hawatapungukiwa na maono, na bado watauweka ukweli katika matendo bila kufeli katika ushuhuda wao. Wao ndio watakaosimama mwishowe kutoka kwenye taabu kubwa.
2 Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya yanaweza kumshawishi binadamu kikamilifuHafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili