44 Anga Hapa ni Samawati Sana

I

Hii hapa anga, anga iliyo tofauti sana!

Harufu ya kupendeza inasambazwa kote kwenye nchi,

na hewa ni safi.

Mwenyezi Mungu alikuwa mwili na anaishi miongoni mwetu,

Akionyesha ukweli na kuanza hukumu ya siku za mwisho.

Maneno ya Mungu yanaweka wazi ukweli wa upotovu wetu.

Tunatakaswa na kuokolewa

kupitia kila aina ya jaribio na usafishaji.

II

Tunayaaga maisha yetu maovu

na kubadilisha sura yetu ya zamani kuwa sura mpya.

Tunatenda na kuzungumza kwa maadili

na kuruhusu maneno ya Mungu yatawale.

Moto wa upendo wetu kwa Mungu unawashwa mioyoni mwetu.

Tunasambaza maneno ya Mungu, kumshuhudia,

na kusambaza injili ya ufalme.

Tunajitolea nafsi yetu yote kumridhisha Mungu,

na tuko tayari kuteseka maumivu yoyote.

Shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu kwa kubadilisha jaala yetu.

Tunaishi maisha mapya na tunakaribisha kesho mpya kabisa!

Maneno ya Mungu hufunua uweza Wake,

na hushinda na kufanya kundi la washindi.

Wateule wa Mungu kutoka katika mataifa

yote wanarudi mbele ya Mungu.

Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu

na kumwabudu milele.

Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani,

ufalme wa Kristo unatimia duniani.

Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika,

mbingu na dunia zinafanywa upya.

Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya,

na wanaishi katika nuru.

III

Ndugu wanapokutana pamoja,

furaha inaonyesha kwenye nyuso zao.

Tunasoma maneno ya Mungu na kushirikiana ukweli,

tunaungana katika upendo wa Mungu.

Sisi ni watu waaminifu, safi na wazi, hakuna ubaguzi kati yetu.

Tunaishi kwa ukweli, tukipendana,

tukijifunza kutoka kwa nguvu za kila mmoja

na kurekebisha upungufu wetu.

Kwa akili moja tunatimiza wajibu wetu na kutoa dhabihu yetu.

Katika njia ya kwenda katika ufalme,

maneno ya Mungu hutuongoza kupita dhiki na taabu.

Maneno ya Mungu hufunua uweza Wake,

na hushinda na kufanya kundi la washindi.

Wateule wa Mungu kutoka katika mataifa

yote wanarudi mbele ya Mungu.

Watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu

na kumwabudu milele.

Mapenzi ya Mungu yanatendwa duniani,

ufalme wa Kristo unatimia duniani.

Haki na utakatifu wa Mungu vinadhihirika,

mbingu na dunia zinafanywa upya.

Watu wa ufalme wanamwogopa Mungu na kuepuka mabaya,

na wanaishi katika nuru.

Hii hapa anga, anga iliyo tofauti sana!

Iliyotangulia: 43 Maisha Ya Kanisa Ni Ya Kupendeza Sana

Inayofuata: 45 Binadamu Wote Wanakuja Kumwabudu Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki