275 Wimbo wa Onyo Jema

1

Usomaji: Kristo ni mshindi. Kristo ni mshindi.

Kwa kumfuata Mungu na kupata ukweli, unaitembea njia ya uzima.

Kwa kutafuta teolojia na kuhubiri nadharia, unawadhuru wengine na wewe mwenyewe.

Kuhubiri mafundisho na kushikilia sheria kunaonyesha kwamba huna uhalisi.

Kwa kutoa wito kwa sauti na kutotenda, unamdanganya Mungu waziwazi.

Kushindania hadhi na kutafuta umaarufu ni ufidhuli na kujidai.

Kwa kufuata tamaa zako mwenyewe na kukiuka ukweli, unamwasi Mungu.

Kwa kuhodhi mawazo na kumpinga Mungu moyoni mwako, unajiweka dhidi Yake.

Kutokuwa na utambuzi na kumsikiliza kila mtu kunakufanya mpumbavu sana.

Kumwabudu mwanadamu na kufuata mwanadamu kunakufanya mtu asiyeamini.

Huwezi kufikia chochote kwa kutumainia vipaji vyako na kujitegemea.

Kumcha Mungu na kuepuka maovu tu ndiko kunakufanya uwe na hekima.

Kwa kutekeleza wajibu wako kwa kanuni, unapata sifa ya Mungu.

Ee, Kristo ndiye ukweli milele.

Ee, Kristo ndiye ukweli milele.

2

Usomaji: Kristo ni mshindi. Kristo ni mshindi.

Watu waaminifu si wazembe katika wajibu wao.

Watu wadanganyifu wanaweza kufanya juhudi kiasi, lakini hawana uaminifu.

Ukiwa na moyo mzuri na kutenda matendo mema, Mungu hakika atakuokoa.

Ukiwa na moyo mwovu na ubinadamu mbaya, hakika Mungu atakufunua.

Kwa kutafuta neema na kukataa kuhukumiwa, kweli unamsaliti Mungu.

Kwa kutenda maneno ya Mungu na kuwa na uhalisi, hakika Mungu atakubariki.

Kusababisha mgawanyiko na kuwadanganya watu ni matendo ya Shetani.

Kujiimarisha na kuwafanya wengine wakutii ni ufidhuli wa ajabu sana.

Kuwatega wengine kwa hila na kuanzisha ufalme wako kunakufanya uwe pepo mbaya na mpinga Kristo.

Kumfuata Mungu na kuishi kwa maneno Yake kunakufanya uwe mwenye busara kweli.

Kushuhudia kwa Mungu na kumtukuza Mungu ni huduma ya kweli.

Kumpenda Mungu na kutenda ukweli ni njia ya Petro ya mafanikio.

Ee, Kristo ndiye ukweli milele.

Ee, Kristo ndiye ukweli milele.

Iliyotangulia: 274 Tambua Kuwa Kristo Ni Ukweli Milele

Inayofuata: 276 Mfuate Mungu Daima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp