296 Huzuni ya Binadamu Aliyepotoka
1 Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili.
2 Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa.
3 Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili