421 Zungumza kwa Dhati Katika Maombi ili Uwe na Kazi ya Roho Mtakatifu

1 Sala ni ya muhimu sana kwenu. Unapoomba, unapokea kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo moyo wako unaguswa na Mungu, na nguvu za upendo kwa Mungu ndani yako huchipuka. Ikiwa hutaomba kwa moyo wako, ikiwa hutafungua moyo wako kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi ndani yako. Hakuna mtu anayeweza kuwa bila mawasiliano ya karibu na Mungu. Bila sala, unaishi katika mwili, unaishi katika utumwa wa Shetani; bila sala ya kweli, unaishi chini ya ushawishi wa giza. Natumaini kwamba ndugu wanaweza kuomba kila siku. Huku si kuzingatia mafundisho ya dini, hata hivyo, bali matokeo ambayo yanapaswa kutimizwa.

2 Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako.

3 Kigezo cha chini kabisa cha sala ni kwamba lazima uweze kuuweka moyo wako kwa amani mbele za Mungu, na hupaswi kuondoka kwa Mungu. Pengine, wakati huu, hujapata mtazamo mpya au wa juu, lakini lazima utumie sala ili mambo yaendelee kama yalivyo—huwezi kurudi nyuma. Hili ndilo jambo dogo zaidi ambalo unapaswa kutimiza. Kuingia kwako katika maisha ya kiroho kunadhihirishwa na iwapo sala zako zimeingia katika njia sahihi au la. Watu wote lazima waingie katika uhalisi huu, lazima wafanye kazi ya kujifunza wenyewe kwa kufahamu katika sala, sio kusubiri kwa kukaa tu, lakini kwa ufahamu watafute kuguswa na Roho Mtakatifu. Wakati huo tu ndipo watakuwa watu wanaomtafuta Mungu kwa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 420 Athari ya Maombi ya Kweli

Inayofuata: 422 Maombi ya Unyenyekevu na Busara Ni ya Umuhimu Mkubwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp