663 Unapaswa Kusimama Upande wa Mungu Majaribio Yafikapo

1 Uzoefu wako mwingi wa kushindwa, udhaifu, nyakati zako za uhasi, vyote vinaweza kusemekana kuwa majaribu ya Mungu. Hii ni kwa sababu kila kitu hutoka kwa Mungu, na mambo yote na matukio yako katika mikono Yake. Kama unashindwa au kama wewe ni dhaifu na unajikwaa, yote yako kwa Mungu na vipo katika mfumbato Wake. Kutoka kwa mtazamo wa Mungu, haya ni majaribu yako, na kama huwezi kutambua hivyo, yatageuka majaribu. Kuna aina mbili za hali ambazo watu wanapaswa kutambua: Moja inatoka kwa Roho Mtakatifu, na chanzo cha nyingine huenda ni Shetani. Moja ni hali ambamo Roho Mtakatifu anakuangazia na Anakuruhusu upate kujijua mwenyewe, kuchukia na kuhisi majuto kujihusu mwenyewe na kuweza kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu, kuweka moyo wako katika kumridhisha Yeye. Nyingine ni hali ambamo unajijua mwenyewe, lakini wewe ni hasi na dhaifu. Inaweza kusemwa pia kuwa hii ni hali ya usafishaji wa Mungu, na pia kuwa ni ushawishi wa Shetani.

2 Ukitambua kuwa huu ni wokovu wa Mungu kwako na ukihisi kuwa wewe sasa ni mdeni Wake mkubwa, na kama kuanzia sasa utajaribu kulipa deni Lake na usianguke tena katika upotovu kama huo, kama utaweka juhudi katika kula na kunywa maneno Yake, na kama siku zote unajichukua kama anayekosa, na kuwa na moyo wa hamu, basi haya ni majaribu ya Mungu. Baada ya mateso kumalizika na wewe kwa mara nyingine tena unasonga mbele, Mungu bado atakuongoza, atakuangazia, atakupa nuru, na kukusitawisha. Lakini kama hulitambui na wewe ni hasi, kujiachilia tu kukata tamaa, kama unafikiri hivi, basi kishawishi cha Shetani kimekufikia. Wakati Ayubu alipitia majaribu, Mungu na Shetani walikuwa wanawekeana dau, na Mungu alimruhusu Shetani amtese Ayubu. Hata ingawa ilikuwa ni Mungu aliyekuwa anamjaribu Ayubu, hakika alikuwa ni Shetani ndiye aliyemjia. Kwa Shetani, ilikuwa ni kumjaribu Ayubu, lakini Ayubu alikuwa upande wa Mungu. Kama haingekuwa vile, basi Ayubu angeanguka katika kishawishi. Mara baada ya watu kuanguka katika kishawishi, wao huanguka katika hatari. Kupitia usafishaji inaweza kusemwa kuwa jaribu kutoka kwa Mungu, lakini kama hauko katika hali nzuri inaweza kusemwa kuwa kishawishi kutoka kwa Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 662 Anachopaswa Kushikilia Mwanadamu Katika Majaribio

Inayofuata: 664 Mungu Anapoijaribu Imani ya Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp