593 Kipimo cha Mungu cha Kupima Mema na Maovu

1 Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanaonwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu. Fikira zako na matendo ya nje hayashuhudii kwa Mungu, wala hayamwaibishi Shetani au kumshinda; badala yake, yanamwaibisha Mungu, na katika kila kitu ni ishara za kumfanya Mungu aibike. Humshuhudii Mungu, hujitumii kwa ajili ya Mungu, na hutimizi jukumu na wajibu wako kwa Mungu lakini badala yake unatenda kwa ajili yako. Ni nini maana ya “kwa ajili yako”? Kwa ajili ya Shetani.

2 Kwa hiyo, mwishowe Mungu atasema, “Tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Machoni pa Mungu, matendo yako hayajakuwa mema lakini badala yake yamekuwa matendo mabaya. Hakuna thawabu. Mungu hakukumbuki. Je, huu si utupu? Kwa kila mmoja wenu anayetimiza wajibu wake, haijalishi jinsi unavyoelewa ukweli kwa kina, iwapo ungependa kuingia katika uhalisi wa ukweli, basi njia rahisi zaidi ya kutenda ni kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu katika kila kitu unachofanya, na kuachana na tamaa zako za kibinafsi, nia zako binafsi, dhamira, heshima na hadhi. Yaweke maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza—hili ndilo jambo la msingi kabisa unalopaswa kufanya. Ikiwa mtu anayetimiza wajibu wake hawezi hata kufanya kiwango hiki, basi anawezaje kusemwa kuwa anatimiza wajibu wake? Huku si kutimiza wajibu wa mtu.

Umetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 592 Kufanya Kazi kwa Uzembe Si Kutekeleza Wajibu

Inayofuata: 594 Mungu Atawapuuza Wale Wanaokosa Kutenda Wajibu Wao

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp