249 Hadithi ya Tomaso ni Onyo kwa Mwanadamu

Kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.

1 Maneno haya yaliyorekodiwa katika Biblia ambayo Bwana Yesu aliongea Alipojitokeza kwa Tomaso ni msaada mkubwa kwa watu wote katika Enzi ya Neema. Kuonekana Kwake na maneno Yake kwa Tomaso yamekuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo, na yatakuwa na umuhimu wa kudumu daima dawamu. Tomaso anawakilisha mtu wa aina ya kuamini Mungu ilhali anamshuku Mungu. Wao wanayo maumbile ya kushuku, wana mioyo isiyoeleweka, wao wenyewe ni wadanganyifu, na hawaamini mambo ambayo Mungu anaweza kukamilisha. Hawaamini katika kudura ya Mungu na utawala Wake, na hawaamini katika Mungu kuwa mwili. Hata hivyo, kufufuka kwa Bwana Yesu kulikuwa ni sawa na kuzabwa kofi katika nyuso zao, na pia kuliwapa fursa ya kugundua ni shaka yao wenyewe, kutambua kushuku kwao binafsi, na kuukubali udanganyifu wao binafsi na hivyo basi kuamini katika kuwepo na kufufuka kwa Bwana Yesu.

2 Kile kilichomfanyikia Tomaso kilikuwa onyo na tahadhari kwa vizazi vijavyo ili watu wengi zaidi waweze kujitahadharisha na ili wasiwe wa kushuku kama Tomaso, na kama wangekuwa hivyo, wangezama katika giza. Ukimfuata Mungu, lakini kama Tomaso, siku zote unataka kuugusa ubavu wa Bwana na kuhisi alama Zake za msumari ili kuthibitisha, ili kuhakikisha, ili kuchambua kama Mungu yupo, basi Mungu atakuacha. Hivyo basi, Bwana Yesu anawahitaji watu wasiwe kama Tomaso, kuamini tu kile wanachoweza kuona kwa macho yao, lakini kuwa bila kasoro, mtu mwaminifu, kutouwa na shaka yoyote dhidi ya Mungu, lakini kumwamini tu na kumfuata Yeye. Mtu wa aina hii amebarikiwa. Hili ni hitaji dogo sana la Bwana Yesu kwa watu, na onyo kwa wafuasi Wake.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 248 Msingi wa Mungu wa Kuwashutumu Watu

Inayofuata: 250 Hakuna Awezaye Kuelewa Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp