504 Kuteseka kwa Ajili ya Kutenda Ukweli ni kwa Maana Sana

1 Ni kwa sababu Mungu amewafichulia maneno Yake, na hatua yenu ifuatayo ni kuyatenda kwa kweli. Mnapotenda maneno haya, Mungu atatekeleza kazi ya nuru na mwongozo. Hivi ndivyo inavyopaswa kufanywa. Kimsingi kabisa, lengo lenu ni kuacha neno la Mungu lifanye kazi ndani yenu. Yaani, ni kuwa na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu mnapolitenda. Pengine uwezo wenu wa kufahamu neno la Mungu ni duni, lakini unapotenda neno la Mungu, Anaweza kurekebisha dosari hii, kwa hivyo hampaswi tu kujua ukweli mwingi, lakini pia lazima muutende. Hili ni lengo kubwa zaidi ambalo haliwezi kupuuzwa.

2 Yesu alivumilia fedheha nyingi na mateso mengi katika maisha Yake ya miaka thelathini na tatu na nusu. Aliteseka sana kwa sababu tu Alitenda ukweli, alifanya mapenzi ya Mungu katika vitu vyote, na alijali tu mapenzi ya Mungu. Haya yalikuwa mateso ambayo Hangepitia iwapo Angejua ukweli bila kuutenda. Ikiwa Yesu angefuata mafundisho ya Wayahudi na awafuate Mafarisayo, basi Hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu kwa mwanadamu hutokana na ushirikiano wa mwanadamu, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka jinsi Alivyoteseka msalabani ikiwa Hangetenda ukweli? Je, Angesali sala ya huzuni sana kama Hangetenda kulingana na mapenzi ya Mungu? Kwa hiyo, mnapaswa kuteseka kwa ajili ya kutenda ukweli; mtu anapaswa kupitia mateso ya aina hii.

Umetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 503 Unyime Mwili ili Kuona Uzuri wa Mungu

Inayofuata: 505 Kuteseka kwa Ajili ya Kutenda Ukweli Hupata Sifa za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp