651 Kupitia Shida Kuna Umuhimu Mkubwa

1 Ni matarajio yanayokuwa ndani ya mioyo yao wakati wakimsadiki Mungu, matarajio kwamba siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili taabu yao itafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilika na kwamba mateso yao yote yataisha. Fikira hizi zipo katika kina cha mioyo yao kwa sababu mwili wa binadamu hauko radhi kuteseka na unatazamia siku bora zaidi kila unapopitia mateso. Mambo haya hayatafichuliwa bila ya hali sahihi[a]. Wakati hakuna hali yoyote kama hiyo, kila mmoja ataonekana kuwa sawa hasa, ataonekana hasa kuwa na kimo, kuufahamu ukweli kwa kiasi fulani, na kuonekana mwenye nguvu za kipekee. Siku moja, wakati hali fulani itakapoibuka, fikira hizi zote zitajitokeza. Akili zao zitaanza kung’ang’ana, na baadhi yao wataanza kuharibikiwa.

2 Si kwamba Mungu haifungui njia kwa ajili yako, au kwamba Mungu hakupatii neema yake, na bila shaka si kwamba Mungu hakufikirii katika ugumu wako. Ni kwamba kuyavumilia maumivu haya sasa ndiyo baraka yako, kwa sababu lazima ustahimili mateso kama haya ili kuokolewa na kunusurika, na yote haya yamepangiliwa awali. Hivyo kwa mateso haya kukukumba wewe ni baraka kwako. Usifikirie kwamba jambo hili ni rahisi; hili si jambo tu la kuchezea watu na kuwafanya kuteseka; maana yake fiche ni ya kina sana, muhimu sana. Kama njia unayoifuata ni sahihi, kama kile unachotafuta ni sahihi, basi mwishowe kile utakachopata kitakuwa zaidi ya kile ambacho watakatifu wa enzi, na ahadi utakazorithi zitakuwa kubwa zaidi.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 650 Lazima Utambue Maana ya Mateso Yako ya Sasa

Inayofuata: 652 Ninyi Ndio Wale Watakaopokea Urithi wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp