949 Maana ya Ishara ya Ghadhabu ya Mungu
1 Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na hazionekani na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.
2 Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili