666 Kujaribiwa na Maneno ya Mungu ni Kubarikiwa

1 Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii. Watu walikuwa wakisema kwamba hawakustahili kuuona uso wa Mungu au kusikia maneno Yake. Leo ni kwa sababu tu ya kutiwa moyo na Mungu na fadhili Zake ndio watu wamepokea usafishaji wa maneno Yake. Hii ni baraka ya kila mtu ambaye anazaliwa katika siku za mwisho—je, nyinyi binafsi mmepitia haya?

2 Ni katika hali zipi watu wanapaswa kuteseka na kuwa na vipingamizi imekusudiwa na Mungu, na haitegemei mahitaji ya watu wenyewe. Hii ni kweli kamili. Kila muumini anapaswa kuwa na uwezo wa kupitia majaribio ya maneno ya Mungu na kuteseka ndani ya maneno Yake. Je, hili ni jambo mnaloweza kuliona dhahiri? Kwa hiyo kuteseka ulikopitia kumebadilishana na baraka za leo; ikiwa hutateseka kwa ajili ya Mungu, huwezi kupata sifa Zake. Labda umelalamika hapo awali, lakini haijalishi umelalamika kiasi gani Mungu hakumbuki hayo kukuhusu wewe. Leo imekuja na hakuna haja ya kuchunguza masuala ya jana.

Umetoholewa kutoka katika “Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 665 Anachotaka Mungu Katika Majaribio Ni Moyo wa Kweli wa Mwanadamu

Inayofuata: 667 Mwanadamu Haelewi Nia Njema za Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp