Je, Yesu Kristo Ni Mungu au Mwana wa Mungu?

16/08/2019

Na Xie Wen, Japani

Hivi karibuni, wakati ambapo kikundi cha wasomi wa Bibilia kilipokaribia kukunja jamvi, Dada Li, mfanyakazi mwenza, aliuliza swali hili: “Bibilia inarekodi, ‘Na Yesu, baada ya kubatizwa, alitoka majini mara moja: na, tazama, mbingu zikamfungukia, na Akamwona Roho wake Mungu akiteremka kama njiwa, na kuja juu Yake: Na tazama sauti kutoka mbinguni, ikisema, Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye(Mathayo 3:16-17). Na Bwana Yesu alipoomba, aghalabu angesema ‘Mungu Baba,’ kwa hiyo tumekuja kuamini katika mioyo yetu kwamba kuna Mungu Baba aliye mbinguni na Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu. Lakini katika ibada zangu za siku chache zilizopita, niliona kwamba Bwana Yesu alisema, ‘Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja(Yohana 10:30). Na katika Maandiko, Filipo anamsihi Bwana awaonyeshe Baba, na jibu la Bwana Yesu ni, ‘Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi?(Yohana 14:9-10). Ni wazi kwamba Mwana ni Mwana na Baba ni Baba, kwa hiyo wanawezaje kuwa kitu kimoja? Je, Bwana Yesu kweli ni Mungu Mwenyewe au Yeye ni Mwana wa Mungu?” Mimi na wafanyakazi wenza wengine tuliokuwa pale sote tulifikiri kwa makini kuhusu vifungu hivi, lakini hatukuwa na hakika tuseme nini, hivyo tukatamatisha mkutano.

Nilipata simu kutoka kwa Dada Gao siku chache baadaye. Alikuwa amesafiri kwa ajili ya kazi kwa zaidi ya nusu mwaka na ndio kwanza alikuwa amerudi, kwa hiyo alitaka tukutane na kuwa na ushirika. Wazo lilinijia kuwa alikuwa amekuwa mhubiri kwa miaka kadhaa na alikuwa na ufahamu dhahiri kabisa wa Biblia, na wakati huo alipokuwa mbali akihubiri hakika alipata mengi sana. Niliwaza moyoni kwamba ningejadiliana naye kuhusu machafuko niliyoachwa nayo kutoka kwa somo la mwisho la Bibilia na kuona alikuwa na ufahamu wa aina gani. Nilimwomba Dada Song aende pamoja nami kumuona Dada Gao. Tulitaniana kwa muda kidogo, na kisha nikazungumza juu ya utata uliokuwa moyoni mwangu.

Aliposikia haya, Dada Gao alitabasamu na kushiriki ushirika huu nasi: “Ili kuelewa suala hili, kwanza lazima tuelewe marejeo ya ‘Mwana na Baba’ yalitoka wapi. Kwa kweli hayakutokea hadi wakati ambapo Bwana Yesu alikuwa mwili ili kufanya kazi ya ukombozi. Wakati huo, Mungu alichukua umbo la Mwana wa Adamu ili kuongea na kufanya kazi kati ya wanadamu, Akizindua kazi ya Enzi ya Neema.Roho Mtakatifu alitoa ushuhuda wa moja kwa moja kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu alipobatizwa, na Bwana Yesu pia alimtaja Mungu aliye mbinguni kama ‘Baba.’ Hivi ndivyo wazo hili la Mwana na Baba lilivyotokea. Lakini kweli linakubalika? Je, Bwana Yesu kwa kweli ni Mwana wa Mungu? Tukiangalia nyuma, je, Mungu alisema katika Kitabu cha Mwanzo kwamba alikuwa na mwana? Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu aliwahi kusema kupitia manabii Wake kwamba alikuwa na mwana? Hakuwahi kusema, siyo? Hii inaonyesha kuwa kuna Mungu mmoja tu na hakuna kitu kama ‘Mwana na Baba.’ Pia, kama ingekuwa jinsi tunavyoielewa, na Bwana Yesu angekuwa Mwana wa Mungu na Mungu aliye mbinguni angekuwa Baba, basi ukweli kwamba Bibilia inasema wazi wazi kuwa kuna Mungu mmoja tu ungeelezwaje? Kwa miaka elfu mbili zilizopita watu wachache sana wamegundua kweli kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe, na alikuwa kuonekana kwa Mungu! Hebu tufungue Biblia zetu katika kitabu cha Yohana 14:8. Wakati Filipo hakumjua Mungu, alimwambia Bwana Yesu, ‘Bwana, tuonyeshe Baba.’ Je, jibu la Bwana Yesu lilikuwa lipi?”

Dada Song alifungua Bibilia yake na kusoma: “Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo(Yohana 14:9-10).

Dada Gao alisema kwa ukunjufu, “Bwana Yesu alirekebisha kosa la Filipo kwa kusema ‘Yeye ambaye ameniona amemwona Baba,’ na ‘Mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi.’ Tunaweza kuona hapa kuwa Baba ni Mwana, na Mwana ni Baba—Wao ni kitu kimoja. Bwana Yesu hakuwahi kusema kuwa Yeye na Mungu wana uhusiano wa baba na mwana, lakini badala yake aliwaambia watu wazi wazi kuwa Yeye na Baba ni kitu kimoja. Kutoka kwa maneno haya ya Bwana Yesu, tunaweza kudhibitisha kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, kwamba Alikuwa udhihirisho wa Mungu katika mwili.”

Dada Song alisema kwa furaha, “Naam, maneno ya Bwana Yesu yapo wazi kabisa: ‘Mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi,’ na ‘Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja.’ Yeye ni Mungu Mwenyewe! Tumesoma maneno haya kutoka Kwake mara nyingi sana—kwa nini hatujawahi kuyaelewa?”

Nilipokuwa nikisikiza ushirika wa Dada Gao, nilijiwazia, “Ni kweli. Bwana Yesu hakuwahi kusema kuwa Yeye na Mungu walikuwa na uhusiano wa baba na mwana lakini alisema kwamba Walikuwa mamoja. Hii inamaanisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe.” Hata hivyo, bado nilihisi shaka fulani moyoni mwangu na nikauliza, “Kwa kuwa Bwana Yesu ndiye Mungu Mwenyewe, kwa nini Roho Mtakatifu alishuhudia kwamba alikuwa Mwana mpendwa baada ya ubatizo Wake? Na Alipoomba, kwa nini alimwomba Mungu Baba? Hakika kuna siri fulani ndani ya jambo hili, siyo?”

Huku akitabasamu, Dada Gao aliendelea na ushirika. “Uko sahihi; kweli kuna siri zilizomo ndani ya jambo hili. Mungu anapopata mwili, Roho Wake anafichwa ndani ya mwili, na mwili huo hauwezi kuhisi hilo kabisa, kama sisi tu, wanadamu, hatuwezi kuhisi roho zetu ndani yetu wenyewe. Kabla ya Bwana Yesu kuanza kufanya kazi na kutekeleza agizo Lake, Alikuwa akiishi katika hali ya ubinadamu wa kawaida. Hakuwa na habari kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili kwa sababu Roho wa Mungu anapokaa ndani ya mwili ili kufanya kazi, kazi Yake si ya kimwujiza, lakini ni ya kawaida kabisa. Ni kama tu Bibilia inavyosema, ‘Lakini kuhusu siku hiyo na saa hiyo hakuna mwanadamu aijuaye … wala Mwana, bali Baba(Marko 13:32). Bwana Yesu alipochukua nafasi Yake kirasmi, Roho Mtakatifu alitamka maneno ya kushuhudia Mwenyewe kuwa Alikuwa Mungu mwenye mwili, na wakati huo tu ndipo Bwana Yesu alipojua utambulisho Wake wa kweli na kwamba alikuwa amekuja kufanya kazi ya ukombozi. Lakini kabla ya Yeye kusulubishwa msalabani, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, alikuwa Kristo. Ndiyo maana ilikuwa kawaida Kwake kumwomba Baba wa mbinguni, na pia Alikuwa akimwomba Roho wa Mungu kutoka kwa msimamo wa ubinadamu Wake—lilikuwa jambo la kawaida kabisa. Bwana Yesu alipokaribia kusulubiwa pia alimwomba Mungu Baba, na kupitia hili tunaweza kuona unyenyekevu na utiifu Wake.”

Baada ya kusikia ushirika wa Dada Gao, mimi na Dada Song tulitamka sote ghafla, “Kuna siri nyingi sana zilizofichwa zinazohusu Roho Mtakatifu kutoa ushuhuda kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu! Shukrani kwa Bwana—isingekuwa ushirika huu kamwe tusingeelewa jambo hili!”

Baada ya kusikia ushirika wa Dada Gao, mimi na Dada Song tulitamka sote ghafla

Kisha Dada Gao akatoa kitabu kutoka katika mfuko wake kilichoandikwa “Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo” kwenye jalada. Alisema kwa furaha, “Kuna vifungu fulani katika kitabu hiki ambavyo kweli bila shaka vinashughulikia swali hili. Wacha tuvisome!” Alipokuwa akisema hivyo, alifungua kitabu hicho na kusoma kwa sauti: “Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mtu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa ‘Mwana wa Adamu’ jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? ‘Baba Yetu Uliye mbinguni….’ Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu ‘Baba,’ je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti” (“Je, Utatu Upo?”).

Aidha kuna wale wasemao, ‘je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?’ Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, ‘Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,’ hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. … Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia(“Je, Utatu Upo?”).

Alipomaliza kusoma, Dada Gao alishiriki ushirika huu: “Kutoka kwa maneno haya tunaweza kuelewa wazi kuwa Bwana Yesu alipobatizwa na Roho Mtakatifu akashuhudia kwamba alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, huyu alikuwa ni Mungu akizungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho. Na Bwana Yesu Kristo alipokuwa akiomba na kumwita Mungu aliye mbinguni ‘Baba,’ ilikuwa tu Bwana Yesu akimwomba Roho wa Mungu kutoka kwa mtazamo wa mwili. Haithibitishi hata kidogo kuwa Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Mungu aliye mbinguni. Lakini kwa kuwa hatuna hakika kuhusu kipengele hiki cha ukweli na hatuelewi mtazamo ambao Mungu alikuwa akizungumzia kutoka, sisi hutegemea makisio yetu wenyewe kueleza maneno ya Mungu kiholela. Ndiyo maana tumefikia wazo hili kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, lakini halikubaliani hata kidogo na ukweli na hasa halilingani na ukweli. Ni dhahiri kuwa hatumjui Mungu na hatuelewi maana ya kweli ya maneno ya Mungu. Tunategemea tu mawazo yetu, tukimwekea mipaka na kumpinga. Kwa kadiri ya kiwango cha kumjua Mungu, lazima tutafute kabisa kwa mioyo minyenyekevu!”

Niliguswa sana baada ya kusikia vifungu hivyo viwili na ushirika wa Dada Gao. Nilidhani, “Kwa hiyo imetukia kwamba Roho Mtakatifu aliposhuhudia ya kuwa Bwana Yesu alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, Alikuwa akizungumza kutoka kwa mtazamo wa Roho, na Bwana Yesu alipomwita Mungu aliye mbinguni ‘Baba,’ Alikuwa akizungumza kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hatujaelewa siri zinazohusu jambo hili lakini tumechunguza tu na kumwekea Mungu mipaka kulingana na fikira na mawazo yetu wenyewe. Huo ni upumbavu kabisa, upuuzi mtupu!” Nilihisi mwenye hatia kabisa ndani yangu, lakini bado kulikuwa na kitu ambacho kilinitatiza. Niliendelea kuuliza, “Kwa nini Mungu hangeshuhudia moja kwa moja kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Hakika mapenzi mazuri sana ya Mungu yamo ndani ya jambo hili. Je, unaweza kushiriki nasi zaidi kuhusu jambo hili?”

Dada Gao aliendelea na ushirika wake. “Hili ni jambo ambalo nimekuja tu kuelewa kupitia maombi na kutafakari, na pia kutafuta na kufanya ushirika na ndugu wengine. Roho Mtakatifu kutoshuhudia moja kwa moja kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe kweli kuna hekima na mapenzi ya Mungu. Bwana Yesu, ambaye alifanya kazi kati ya wanadamu, kwa kweli alikuwa Mungu akivalia mwili na kuwa mwanadamu, Akija kufanya kazi na kuonekana kwetu. Bila kujali jinsi alivyofanya kazi au kuzungumza, au kumwomba Mungu Baba, kiini Chake kilikuwa cha Mungu, si cha binadamu. Mungu ni Roho na haiwezekani sisi kumuona, lakini unaonaje anapovalia mwili? Tunachoona ni mwili wa nyama; hatuwezi kuona Roho wa Mungu. Iwapo Roho Mtakatifu angeshuhudia kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe ingekuwa ngumu kwetu kukubali, kwa sababu watu wa wakati huo hawakuwa na dhana ya Mungu kuwa mwili. Hawakuwa hasa na ufahamu wa jambo hili kwa kuwa walikuwa ndiyo kwanza wamekutana na Mungu mwenye mwili, na hawangefikiria kamwe kuwa Mwana wa Adamu aliyeonekana wa kawaida kwa kweli alikuwa mfano halisi wa Roho wa Mungu, kwamba alikuwa kuonekana kwa Mungu katika mwili. Kwa hiyo, ingawa Bwana Yesu alisema maneno mengi alipokuwa akifanya kazi, Akatuletea injili ya ufalme wa mbinguni, na kufichua ishara nyingi na maajabu, Akionyesha kikamilifu mamlaka na nguvu ya Mungu, wafuasi Wake hawakugundua kutoka kwa kazi na maneno Yake kwamba alikuwa Mungu Mwenyewe, kwamba Alikuwa udhihirisho wa Mungu. Fikiria nyuma kuhusu hilo—watu wa wakati huo walimwitaje Bwana Yesu?”

Dada Song alisema mara moja, “Bibilia inarekodi, “Wengine husema kwamba wewe ni Yohana Mbatizaji: wengine husema Eliya; na wengine, Yeremia, ama mmoja wa manabii” (Mathayo 16:14).

Dada Gao alithibitisha hili: “Hiyo ni kweli. Ilikuwa kwa sababu watu wa wakati huo walimkubali tu Bwana Yesu kama mmoja wa manabii au walimtaja kama ‘Bwana’—hawakugundua kuwa Alikuwa Mungu katika mwili. Hii ndiyo sababu Mungu aliwaruhusu watu wamwite Bwana Yesu Mwana wa Mungu kwa muda mfupi kulingana na kimo cha watu wakati huo; hakuwasukuma watu zaidi ya uwezo wao, lakini alishuhudia kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu kwa mujibu wa kile ambacho watu waliweza kuelewa. Hilo ndilo jambo pekee ambalo lingepatana na mawazo ya watu na ambalo wangekubali kwa urahisi. Kwa kuwa Alikuwa akifanya kazi ya ukombozi, bila kujali walimwita vipi Bwana Yesu, almradi wakubali wokovu Wake, wakiri na kutubu kwa Bwana, hawangelaaniwa tena chini ya sheria—hiyo ilitosha. Si unaweza kusema kwamba nia njema na hekima ya Mungu ilikuwa imefichwa kuhusiana na yote haya?”

Tuliposikia hivi, mimi na Dada Song tulijipata tukikubali kwa kichwa kwa wakati mmoja hasa. Tuliona kwamba mara kwa mara, Mungu amekuwa akisamehe kabisa asili zetu za utoto na ujinga—Alijua kwamba hatukujua kuhusu Mungu kuwa mwili, kwa hiyo Alitumia njia hiyo kushuhudia ya kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu katika mwili. Hiyo kweli ilikuwa nia nzuri sana na njema ya Mungu!

Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato (Sehemu 1)

Dada Gao aliendelea, akisema: “Roho wa Mungu alipochukua mwili, ingawa hatungeweza kuona Roho Wake, tabia Yake, kile Anacho na Alicho, pamoja na uweza Wake na hekima zote zilionyeshwa kupitia mwili huo. Tunaweza kuthibitisha kikamilifu kutoka kwa kazi na maneno ya Bwana Yesu na tabia aliyoonyesha kuwa Alikuwa Mungu Mwenyewe. Bwana Yesu alitoa habari kwamba ufalme wa mbinguni ulikuwa karibu na akawapa watu njia ya kutubu, Akifungua Enzi ya Neema na kufunga Enzi ya Sheria. Alionyesha tabia yenye wema na huruma, Akifanikisha kazi ya kuwakomboa wanadamu. Je, si kazi hii yote ilikuwa kitu ambacho Mungu Mwenyewe pekee angeweza kufanya? Aidha, maneno Yake yalikuwa yamejaa mamlaka na nguvu—Alichosema kilitokea, na kile alichoamuru kilitimia. Neno lolote ambalo lilitoka kwa kinywa Chake kwa kweli lilitimizwa. Bwana Yesu aliweza kumsamehe mtu dhambi zake, kutuliza bahari zenye dhoruba, na kumfufua mtu kutoka kwa wafu Akitumia maneno machache rahisi. Kutokana na kazi na maneno ya Bwana Yesu, tuliona mamlaka na nguvu ya Mungu katika utawala Wake juu ya vitu vyote, na pia tuliona uweza, hekima na matendo ya Mungu ya ajabu. Kazi na maneno yote ya Bwana Yesu yalikuwa maonyesho ya moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu—si hiyo inathibitisha kwamba alikuwa Roho wa Mungu katika mwili, Akizungumza moja kwa moja na wanadamu, Akifanya kazi kati ya wanadamu, na kuonekana kwa wanadamu? Je, si ungesema kuwa kile ambacho Bwana Yesu alifanya kilikuwa kazi ya Mungu Mwenyewe?”

Baada ya kusikia haya, nilikubali kwa kichwa na nilihisi hakika ndani ya moyo wangu kuwa Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi ya Mungu Mwenyewe, kwamba kweli alikuwa Mungu Mwenyewe. Huku nikihisi aibu, nilishiriki ushirika huu na Dada Gao na Dada Song: “Nimekuwa nikimwamini Bwana miaka hii yote na nimefurahia baraka nyingi sana na neema nyingi sana kutoka Kwake, lakini sikuwahi kugundua kuwa Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe, kwamba alikuwa kuonekana kwa Mungu. Nimekuwa daima na wazo kwamba alikuwa Mwana wa Mungu, kwa hiyo sikuwahi kumtazama kama Mungu Mwenyewe. Sasa naelewa—Bwana Yesu Kristo alikuwa Mungu Mwenyewe, na Alikuwa kuonekana kwa Mungu. Utata huu ambao nimekuwa nao moyoni mwangu hatimaye umesuluhishwa—nashukuru sana kwa ajili ya mwongozo wa Bwana!”

Dada Song alisema kwa aibu, “Tunamwamini Bwana lakini hatumjui kabisa, na hatuna ufahamu hata kidogo kuhusu siri za ukweli wa kupata mwili. Ninapofikiri kuhusu ukweli kwamba nimekuwa muumini kwa miaka hii yote lakini nimeamini tu katika jina la Bwana Yesu bila kuelewa asili Yake ya Mungu, ninahisi mwenye aibu sana, wa kusikitisha na kipofu!”

Kisha nikakumbuka maneno hayo ambayo Dada Gao alikuwa ameyasoma na nikahisi kwamba kitabu hicho, Kitabu Chafunguliwa na Mwanakondoo, lazima ni cha thamani sana na kina uwezo wa kutatua utata na matatizo yetu. Nilisema kwa haraka, “Dada Gao, ninaweza kukaa na kitabu hiki kwa siku chache? Ninathamini sana mambo ambayo yamo ndani yake—yanatoka kwa Roho Mtakatifu. Ningependa pia kaka na dada zangu kanisani wasikie kile ulichosoma leo ili utata wao uweze pia kutatuliwa.”

Dada Gao alikubali kwa shauku kubwa, akisema “Hiyo ni kweli kabisa. Mapenzi ya Mungu na siri za kazi Yake zimewekwa wazi sana katika kitabu hiki. Sio kitu ambacho mtu wa kawaida angeweza kukiandika—hakika kimetoka kwa Roho Mtakatifu. Ningependa pia kukiangalia kwa makini.”

Huku akitabasamu, Dada Gao alisema, “Hamna shida. Maudhui yake kweli yanaadilisha—hebu tuwakutanisheni ndugu kutoka kanisani waweze kukiangalia.”

“Ee, vizuri sana! Mshukuru Bwana!”

“Mshukuru Bwana!” …

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Na Jingmo, MalaysiaNilikuwa na bahati katika mwaka wa 1997 kukubali injili ya Bwana Yesu na nilipobatizwa, mchungaji aliomba na kunibatiza...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp