Pigo Limekuja: Mkristo Anapaswa Kutubu Vipi ili Apate Ulinzi wa Mungu?

29/07/2020

“Virusi vipya vya corona”—maneno yanayotia hofu ndani ya mioyo ya watu—viliibuka mara ya kwanza mjini Wuhan, Uchina, na kutoka hapo vimeenea duniani kote. Watu wanafariki kwa idadi kubwa kote ulimwenguni na wengi zaidi wako katika hali ya hofu daima, wakihisi kwamba misiba mikuu imetufikia. Hakuna mtu anayejua maradhi haya yatadumu kwa muda upi ama yatafisha idadi ipi ya watu. Hata hivyo, wale wanaomwamini Mungu wanajua mioyoni mwao kwamba mambo yote yanatendeka kwa idhini ya Mungu, na kwamba hakuna jambo hata kidogo linaloweza kutendeka bila idhini hiyo. Kwa hivyo, mapenzi ya Mungu katika kuruhusu pigo hili litufikie ni yapi?

Angalia Nyuma Katika Historia na Utafute Mapenzi ya Mungu

Agano la Kale limerekodi kwamba watu wa Sodoma walikuwa waovu, wazinzi na wapotovu, na kwamba mji huo ulikuwa umejaa mauaji na maangamizi, kiasi kwamba watu waliokuwa hapo hata walitaka kuwaua malaika. Hawakuwahi hata kufikiria kutubu, na kwa hivyo Mungu aliwanyeshea moto kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote. Hata hivyo, wale wenye maarifa mengi ya Biblia wanajua kwamba kabla ya Mungu kuuletea mji huo janga, Abrahamu alimsihi Mungu kwa niaba ya Sodoma. Hii ni sehemu ya rekodi hii kutoka katika Biblia: “Na Yehova akasema, Nikipata katika Sodoma watu hamsini wenye haki ndani ya mji huo, basi nitaacha pahali pote kwa sababu yao. … Na akasema, … Iwapo watapatikana huko watu kumi. Naye akasema, Sitauharibu kwa sababu yao(Mwanzo 18:26-32). Mistari hii inafichua tabia ya Mungu yenye haki na hata zaidi inatujulisha rehema na huruma kubwa ya Mungu. Mungu angeusamehe Sodoma iwapo watu hamsini wenye haki wangepatikana hapo, na pia Angeusamehe mji huo iwapo watu kumi tu wenye haki wangepatikana. Licha ya jinsi watu walivyokuwa wapotovu na waovu kwa kina, Mungu bado alitumai kwamba wangetubu. Ni jambo la uchungu kwamba hata watu kumi wenye haki hawangepatikana katika mji mkubwa hivyo, na kwa hivyo hatimaye Mungu hakuwa na chaguo ila kuuharibu.

Watu wanaoishi katika dunia hii sasa, iliyojaa ushawishi, ni wabaya hata zaidi kuliko watu wa Sodoma miaka hiyo yote iliyopita. Watu leo wamepotoshwa kabisa na Shetani. Wanapenda uovu mno na wanapenda udhalimu; ulimwengu umejaa vurugu na uzinzi, na unaweza kuona baa za karaoke, vyumba vya kukanda miguu, hoteli, na vilabu vya kudansi kila mahali katika mitaa mikuu mizima na vichochoro vidogo. Sehemu kama hizi zimejaa uovu na uzinzi. Kila mtu anaishi kwa ajili ya kula, kunywa, kujiburudisha, na kujifurahisha na anasa za mwili, wakiwa wamepotoka mno. Hakuna upendo kati ya watu, lakini kila mtu huhadaana, kushindana na kuchuana kwa ajili ya hadhi, umaarufu na mali; wao hudanganyana na kufanyiana njama, na hata wanapigana kwa ajili ya fedha na faida. Wanadamu wote wanamilikiwa na Shetani, na hakuna mtu anayependa mambo chanya, ama anayetamani sana mwanga, ama anayejitokeza kukubali neema ya wokovu wa Mungu. Hata waumini wanaishi katika mzunguko wa kutenda dhambi na kukiri, wasiweze hata kidogo kushikilia mafunzo ya Bwana. Hata wanafika kiwango cha kufuata mitindo ya dunia na kufuatilia anasa za mwili. Hata wanapojua kwamba wanaishi katika dhambi, bado hawawezi kutupilia mbali vifungo vya dhambi—mioyo yao imepotoka sana kutoka kwa Mungu. Je, wanadamu wote waliopotoka mno hawakufikia hatua ambapo walipaswa kuangamizwa kitambo sana?

Mungu Anatumai Kwamba Watu Wanaweza Kutubu

Misiba inatokea mmoja baada ya mwingine, na mapenzi ya Mungu ni sisi tuje mbele Zake kutubu. Anamtaka kila mtu atubu na hamtaki mtu yeyote aangamie. Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Wakati huu, wengine wenu wanaweza kusema, “Wasioamini hawamwamini Mungu na hawawezi kutubu. Hata hivyo, baada ya kumwamini Bwana, mara nyingi sisi hulia kwa uchungu mbele Zake tunapoomba. Tunakubali dhambi zetu za awali, na hatukosei tena. Tunaweza kuwa wastahimilivu na wenye subira kwa wengine. Tunaweza kutoa ili kuwasaidia wenye shida na kutoa msaada na kuwaauni wengine, hata tunaweza kutumia muda wetu wote kujitahidi na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, na hatutamsaliti Bwana hata tukikamatwa na kutiwa gerezani. Je, hii si toba ya kweli? Tukitenda kwa njia hii kwa uthabiti, basi Bwana atatulinda na kutuzuia tusiangamizwe na misiba.” Lakini mambo yako hivi kweli? Bwana Yesu aliwahi kusema, “Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8: 34-35). Baada ya sisi kumwamini Bwana, tunaweza kuwa wanyenyekevu na wenye subira, tunaweza kuwaauni wengine, na tunaweza kujitolea, kujitumia, kuhubiri injili, kumshuhudia Bwana na tuna mienendo fulani mizuri ya nje. Hata hivyo, hatuwezi kukana kwamba tabia potovu zilizo ndani yetu, kama vile ufidhuli, majivuno, upotovu, udanganyifu, ubinafsi na fedheha hazijatakaswa, na bado tunaweza kutenda dhambi kila mara. Kwa mfano, tunajua vyema kwamba Bwana anatutaka tuwe waaminifu, lakini huku tukidhibitiwa na asili yetu yenye kustahili dharau na yenye ubinafsi, punde tu kitu fulani kinapoingilia maslahi yetu wenyewe, hatuwezi kujizuia kusema uongo na kujihusisha katika udanganyifu; huku tukidhibitiwa na asili yetu fidhuli na ya majivuno, daima tunawafanya wengine wafanye tunachosema bila kujali ni nini, na wasipofanya hivyo tunakasirika na kuwakemea; na misiba na majaribu yanapotukumba, tunalalamika na kumlaumu Bwana. Hii ni mifano michache tu. Dhambi zetu ni kama magugu—zinarudi tu baada ya kuondolewa. Hata tukilia kwa uchungu kila siku tunapoomba na kukiri dhambi zetu, bado hatubadiliki. Je, hii inaweza kuwa toba ya kweli? Ni nani anayeweza kutoa uhakikisho kwamba Mungu atamlinda mtu kama huyu katikati ya misiba? Toba ya kweli ni wakati tabia potovu za mtu za kishetani zinatakaswa na kubadilishwa kikamilifu, wakati hafanyi maovu, kutenda dhambi ama kumpinga Mungu tena. Ni wakati anaweza kumtii Mungu kwa kweli na kumwabudu Mungu. Ni watu kama hawa pekee ndio wanafaa kurithi ahadi na baraka za Mungu na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Jinsi tu Biblia inavyosema: “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). “Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake(Ufunuo 22:14).

Jinsi ya Kutimiza Toba ya Kweli na Kupata Ulinzi wa Mungu

Jinsi ya Kutimiza Toba ya Kweli na Kupata Ulinzi wa Mungu

Basi tunaweza kutimizaje toba ya kweli? Bwana Yesu aliwahi kusema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli(Yohana 17:17). Bwana alitabiri kwamba Atarudi katika siku za mwisho, kwamba Ataonyesha ukweli zaidi na wa juu zaidi kuliko wakati wa Enzi ya Neema, na kwamba Atatekeleza hatua ya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu. Hili ni ili tuweze kuwekwa huru kutokana na vifungo vya dhambi milele na tutakaswe na kubadilishwa. Kwa sababu kazi ambayo Bwana Yesu alifanya katika Enzi ya Neema ilikuwa kazi ya ukombozi, watu wangesamehewa dhambi zao kwa kumwamini. Hata hivyo, watu hawakutakaswa asili yao ya dhambi. Ni kwa kukubali kazi ya Bwana katika siku za mwisho, tutakaswe na kubadilishwa tabia zetu potovu, na tusifanye maovu, kutenda dhambi ama kumpinga Mungu tena tu ndiyo tunaweza kusemekana kuwa tumetubu kwa kweli. Ni hapo tu ndipo tutapata ulinzi wa Mungu na kuendelea kuishi baada ya misiba.

Bwana Yesu amerudi tayari. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Mwenyezi Mungu—Kristo wa siku za mwisho—anatekeleza kazi ya hukumu akianzia na nyumba ya Mungu kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali…. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Ili kutuokoa kutoka kwa minyororo ya tabia zetu za kishetani, Mwenyezi Mungu aonyesha ukweli wote unaoweza kututakasa na kutuokoa kikamilifu. Anafunua siri za kazi ya Mungu ya usimamizi ya miaka elfu sita; Anafichua chanzo cha uovu wa dunia, na pia kiini na ukweli wa wanadamu kupotoshwa na Shetani. Kwa kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, tunaona jinsi tulivyopotoshwa kwa kina na Shetani. Ufidhuli, majivuno, ubinafsi, fedheha, upotovu, udanganyifu, ulafi, uovu—hakuna tunachoishi kwa kudhihirisha kinachofanana na ubinadamu hata kidogo, na hili linachochea Mungu kutuchukia na kuwa na kinyongo nasi. Wakati uo huo, tunakuja kujua tabia ya Mungu yenye haki ambayo haivumilii kosa. Tunatambua kwamba daima tunaishi kulingana na tabia zetu potovu za kishetani, na kwamba tusipotenda ukweli, basi hakika Mungu atatuchukia sana na kutukataa. Ni hapo tu ndipo tunasujudu mbele za Mungu na kutubu. Tunachukia dhambi zetu na tunatamani kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Kwa kuinyima miili yetu mara kwa mara na kutenda ukweli, tabia zetu potovu zinatakaswa na kubadilishwa polepole. Hatumwasi ama kumpinga Mungu tena, na tunaanza kumtii Mungu kwa kweli na kumcha. Ni watu kama hawa tu ndio wale walio na toba ya kweli na watalindwa na Mungu na kuendelea kuishi baada ya misiba.

Mwenyezi Mungu alionekana na kuanza kazi Yake miaka 30 iliyopita. Kazi ya injili imeenea mbali hadi kwa kila taifa ulimwenguni, na mamilioni ya maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu yamechapishwa mtandaoni kitambo. Maneno haya yametafsiriwa katika zaidi ya lugha 20; yanashuhudia na yanapatikana waziwazi kwa wanadamu wote. Katika enzi hii ya kiza na ovu kabisa, ukweli ulioonyeshwa na Kristo wa siku za mwisho unatokea kama mwanga wa kweli, kama umeme, unaowaka kutoka Mashariki hadi Magharibi. Yanatoa ushuhuda kwa wanadamu wote: Mungu ameonekana na Bwana Yesu amerudi. Anaonyesha ukweli ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu, na njia ya pekee ya mwanadamu kupata wokovu kamili ni kumkubali Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, wanadamu wamepotoshwa kwa kina sana na Shetani. Hakuna mtu anayependa ukweli. Watu wanataka tu kutamani anasa za dhambi. Hawataki kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ama kukubali hukumu na kuadibu Kwake katika siku za mwisho. Badala yake, watu wana fikira zilizokita mizizi kuhusu kazi ya Mungu, na wengine hata wanapinga na kushutumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho hadharani. Kila mtu anaishi ndani ya dhambi bila kufikiria kutubu. Wachache mno wanatamani sana ukweli ama kutamani mwanga. Misiba tunayoona leo ni kumbusho la mwisho la Mungu, onyo Lake la mwisho kwa wanadamu. Zaidi ya hayo, ni wokovu wa Mungu. Ni kwa kuja mbele za Mungu kutubu pekee ndiyo tunaweza kupata ulinzi wa Mungu kutokana na misiba.

Tilia Maanani Maonyo ya Mungu

Mwenyezi Mungu anasema, “Maafa yote yatatokea moja baada ya nyingine; mataifa yote na maeneo yote yatapitia maafa—tauni, njaa, mafuriko, ukame na matetemeko ya ardhi yatakuwa kila mahali. Maafa haya hayatokei tu sehemu moja au mbili, wala hayataisha kwa siku moja au mbili, lakini badala yake yataeneza juu ya eneo kubwa zaidi na zaidi, na maafa yatakuwa makali zaidi na zaidi. Wakati huu kila namna ya wadudu tauni watatokea kwa mfululizo, na tukio la watu kuwala watu litatokea kila mahali. Hii ni hukumu Yangu juu ya mataifa yote na watu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 65). “Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). “Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako).

Misiba inazidi kuwa mibaya zaidi duniani kote, ikienea katika maeneo makubwa zaidi. Wale ambao wameandikiwa maangamizo hawawezi kutoroka, na inaonekana kana kwamba mwisho wa dunia utatufikia punde. Hata hivyo, sote tunajua kwamba Mungu anatawala majaliwa yetu na misiba yote iko mikononi Mwake. Tukija mbele za Mungu kutubu na tukubali hukumu na kuadibu Kwake katika siku za mwisho tu ndiyo tutakuwa na fursa ya kulindwa na Mungu kutokana na misiba na tuendelee kuishi. Jinsi dunia inavyoenda inaonekana wazi wazi mbele yetu. Punde Mungu atakapowaokoa wale wote Anaoweza kuokoa, Atatumia misiba mikuu kuharibu dunia hii ovu na chafu. Wakati huo utakapofika, wale ambao hawajakuja mbele za Mungu wataangamizwa na misiba, wakilia na kusaga meno yao.

Maelezo ya mhariri: Baada ya kusoma makala haya, je, sasa waelewa mapenzi ya Mungu ya kuachilia huru misiba ni yapi? Na, je, sasa umepata njia ya kulindwa na Mungu kutokana na misiba? Ikiwa una maswali ama matatizo yoyote zaidi, unakaribishwa kutujulisha wakati wowote kupitia vipengele vya kuzungumza na kupitisha ujumbe kwenye tovuti yetu na kuwasiliana nasi.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Je, Maafa Yatakapofika, Utakuwa Umetimiza Toba ya Kweli?

Siku, maangamizi ya ulimwengu yanapokua makali zaidi, unabii wa kuja kwa Bwana umetimia. Bwana Yesu alisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Toba ya kweli ni nini hasa? Na tunawezaje kutimiza toba ya kweli? Makala haya yatakuambia majibu.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp