Wokovu ni Nini? Je, Wokovu Ndicho Kitu Pekee Kinachohitajika Ili Kuingia Katika Ufalme wa Mbinguni?

11/06/2020

Na Shen Qingqing, Korea Kusini

Watu wengi hutazamia kuokolewa na Bwana wakati wa kuwasili Kwake na kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Leo hii, ni Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee ndilo ambalo limekuwa likishuhudia wazi wazi kwamba Bwana Yesu amerudi, na kwamba Anafanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu kuwaokoa na kuwatakasa watu. Wengine wanaweza kuhisi kuchanganyikiwa wanaposikia habari hii. Wanasoma vifungu vifuatavyo: “Yule ambaye anaamini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule ambaye haamini atahukumiwa(Marko 16:16), “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10), na wanaamini kwamba vinamaanisha ya kuwa kwa sababu Bwana Yesu alisulubiwa ili kulipia dhambi za wanadamu wote, ya kwamba mradi wamwamini Bwana, wataokolewa, na kwamba mara tu wanapookolewa, watakuwa wameokolewa milele. Wanaamini kwamba mradi walishikilie jina la Bwana na wavumilie hadi mwisho, wanaweza kunyakuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi bila kuhitajika kukubali kazi ya Mungu ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho. Je, imani za aina hii ni sahihi?

Acha tuzingatie hili: Je, Bwana aliwahi kusema kwamba mara mtu akishaokolewa anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni? Je, imesemwa hivyo katika Biblia? Jibu la maswali haya yote ni dhahiri sivyo. Bwana Yesu alisema, “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Kwa msingi wa neno la Mungu, tunajua kwamba ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni tu ndio watakaoingia katika ufalme wa mbinguni. Kufanya mapenzi ya Baba wa mbinguni kunamaanisha kuwa na uwezo wa kutia neno la Mungu katika vitendo, kumtii Mungu, na kuweza kuishi kulingana na neno la Mungu bila kujali hali yoyote, na kutotenda dhambi au kumpinga Mungu tena. Ilhali tunaendelea kusema uwongo na kufanya dhambi bila kukusudia, na hata tunashindwa kuweka mafundisho ya Bwana katika vitendo, hivyo basi mtu ambaye bado anaweza kutenda dhambi na kumpinga Bwana kwa namna hii anaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni? La kusikitisha ni kwamba, imani yetu kwamba “ukiokoka mara moja umeokolewa milele” ni ya makosa. Linapokuja suala muhimu la kuingia katika ufalme wa Mungu, lazima tufuate neno la Bwana. Hatuwezi kufuata maoni na mawazo ya mwanadamu! Hivyo maana ya kweli ya “wokovu” katika maandiko ni ipi hasa? Mtu anaingiaje katika ufalme wa mbinguni kwa kweli? Haya ndiyo maswali ambayo tutajadili na kuyachunguza pamoja.

Maana ya Kweli ya “Wokovu”

Sote tunajua ya kwamba mwishoni mwa Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wanazidi kupotoshwa kwa kina na Shetani. Watu wa Israeli mara nyingi walikiuka sheria na amri na walikuwa wakitenda dhambi zaidi na zaidi—nyingi kiasi kwamba hakuna kiwango cha dhabihu kilitosha, na wote walikabiliwa na hatari ya kushutumiwa na kuhukumiwa kifo na sheria. Ili kuwaokoa wanadamu kutokana na tishio la kifo, Mungu alishuka duniani katika mwili kama Bwana Yesu kufanya kazi ya ukombozi, kusulubiwa kwa ajili ya mwanadamu, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya wanadamu wote, na kusamehe dhambi za mwanadamu kabisa. Tangu wakati huo, mradi mtu anaamini katika Bwana Yesu, anakiri dhambi zake kwa Bwana na kutubu, atasamehewa dhambi zake na afurahie baraka na neema zote zilizotolea na Bwana Yesu. Kwa watu walioishi chini ya sheria, huu ulikuwa “wokovu.” Kwa hivyo, “wokovu” ambao Bwana Yesu alizungumzia sio jinsi tunavyofikiria, kwamba mradi tunamwamini Bwana Yesu, tutaokolewa kabisa; badala yake, unamaanisha kuwa watu wanaotenda dhambi hawatashutumiwa na kuhukumiwa kifo na sheria tena, na dhambi za mwanadamu zitasamehewa. Acha tuangalie kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)).

Tunapoamini katika Bwana, hata ingawa tunapokea zawadi ya wokovu na dhambi zetu zinasamehewa, hatufunguliwi kutoka katika minyororo ya dhambi na tunaendelea kuishi katika dhambi. Baadhi ya mifano ya hii ni: Tunaweza kuwa wenye kiburi kupindukia, tukitaka kila mara kuwa na usemi wa mwisho katika hali yoyote ya kikundi na kuwafanya watu wengine wafuate kile tunachosema, na mtu asipokubaliana na kile tunachosema, tunaweza kupatwa na hasira na kumkaripia, na katika hali mbaya zaidi, tunaweza kumwadhibu au kumdhulumu kwa njia fulani. Tunaweza kuwa wabinafsi kupindukia na kutegemeza kila kitu juu ya kanuni ya masilahi ya binafsi, na hata kujaribu kufanya makubaliano na Mungu katika imani yetu Kwake; wakati mambo yako shwari na yanakwenda vizuri, tunamshukuru, lakini tunapokabiliwa na vipingamizi na kutofaulu, tunajawa na suitafahamu na malalamiko Kwake, na hata tunakwenda kiasi cha kumsaliti na kumtelekeza. Tunaweza kuwa wadanganyifu wa ajabu sana, kwamba kila ambapo masilahi yetu ya kibinafsi yanahusika, tunasema uwongo na kudanganya licha ya sisi wenyewe. Hii ni mifano michache tu ya namna tunavyoendelea kuishi katika dhambi. Biblia inasema, “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi, lakini kuitafuta kwa hofu hukumu na uchungu mkali, ambao utawala maadui(Waebrania 10:26–27). “Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34–35). Mungu ni mtakatifu. Baada ya kujifunza kuhusu njia ya kweli, bado tunaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu licha ya sisi wenyewe. Hiyo inamaanisha kuwa sisi ni watumishi wa dhambi, na hatuwezi kupongezwa na Mungu. Biblia inasema, “Bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). Kama mtu hajatakaswa dhambi zake, na mara nyingi anatenda dhambi na kumpinga Mungu, je, mtu huyu anaweza kuokolewa milele? Je, mtu huyu anaweza kustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni? Ni wazi kwamba hawezi. Ni baada tu ya kutakaswa kabisa kutokana na dhambi zetu ndiyo tunaweza kuwa watakatifu na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Na sasa wengine wanaweza kuuliza: Tunaweza kutakaswaje ili tuweze kuingia katika ufalme wa mbinguni?

Tunaweza Kupokeaje Wokovu na Tuingie Katika Ufalme wa Mbinguni?

Tunaweza Kupokeaje Wokovu na Tuingie Katika Ufalme wa Mbinguni?

Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Kutoka katika hili tunaweza kuelewa kwamba ili kutatua tabia ya kishetani iliyokita mizizi ndani ya mwanadamu na kumkomboa kabisa mwanadamu kutokana na minyororo ya dhambi, ni muhimu kwa Bwana kurudi katika siku za mwisho kutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, na kuonyesha ukweli ili Awatakase na kuwaokoa wanadamu. Kwa kweli, Bwana tayari alitabiri hili zamani, kama inavyosema katika Biblia: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12–13). “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17).

Leo, kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Mwenyezi Mungu anatekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, na Anaonyesha ukweli wote wa kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu ili kutatua asili ya dhambi ya mwanadamu kabisa na kumwokoa kutokana na minyororo ya dhambi, Akimtakasa, mpaka mwishowe apatwe na Mungu na kuongozwa kuingia katika ufalme wa Mungu. Kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho inatimiza unabii huu kikamilifu. Wale wote wanaiokubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho watapokea utakaso na wokovu wa Mungu. Wote watakuwa na fursa ya kufanywa kuwa washindi kabla ya maafa makubwa kufika, kutukuzwa pamoja na Mungu, na kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Hivyo, Mwenyezi Mungu huwahukumu na kuwatakasaje watu na kuwaokoa kutokana na minyororo ya dhambi?

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Inaweza kuonekana kutoka katika haya kwamba Mungu hutumia ukweli mwingi kuhukumu na kufunua tabia ya kishetani ya kumwasi na kumpinga Mungu. Tunapopitia hukumu ya maneno ya Mwenyezi Mungu, sisi binafsi tunaona kuwa tabia ya Mungu yenye haki haivumilii kosa lolote. Kila neno la Mungu hupenyeza ndani ya mioyo yetu na kufunua kila aina ya udhihirisho wa upotovu, na vile vile fikira na mawazo yasiyofaa, nia chafu, na maoni na fikira zilizo ndani ya mioyo yetu, na vile vile asili ya Shetani iliyo katika vitu hivi, na hivyo kutufanya tudhalilishwe na aibu na kuwa wenye kujaa majuto sana kwamba tunaanguka mbele za Mungu na kutubu Kwake kwa kweli. Wakati huo huo, Mungu pia Anatuonyesha njia za kutenda, kama vile ni maoni gani tunayopaswa kuwa nayo katika imani yetu kwa Mungu, jinsi ya kuwa mtu mwaminifu, jinsi ya kumtukuza na kumshuhudia Mungu, jinsi ya kuepuka kuitembea njia ya mpinga Kristo, jinsi ya kufanikisha utiifu wa kweli kwa Mungu na upendo wa kweli kwa Mungu, na kadhalika. Ni wakati tu ambapo tumepitia kazi ya hukumu ya Mungu na tunatenda kulingana na maneno ya Mungu ndipo tunaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Haya yote ni matokeo ya hukumu ya Mungu.

Leo, ushuhuda wa matukio ya kila aina kutoka kwa ndugu wengi katika Kanisa la Mwenyezi Mungu ambao wamepitia hukumu sasa umechapishwa kwenye mtandao. Kutoka kwa matukio haya ya kweli na ushuhuda, inaweza kuonekana kwamba ni kwa kupitia tu kazi ya kuadibu na hukumu ambayo Mungu anafanya katika siku za mwisho ndiyo mtu anaweza kutakaswa na kupatwa kabisa na Mungu—hii ndiyo njia pekee ya sisi kufika katika ufalme wa mbinguni. Kufikia sasa, watu wengi kutoka ulimwenguni kote wanaomwamini Mungu kweli wamepata njia ya kuingia katika ufalme wa mbinguni kupitia katika maneno ya Mwenyezi Mungu na wamerejea Kwake. Tukiendelea kushikilia wazo la “ukiokoka mara moja umeokolewa milele” na tusiikubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, tabia zetu potovu hazitatakaswa na kubadilishwa, na hivyo, hatutakuwa kamwe na nafasi ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hivyo, bado unangoja nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kuokolewa ni nini? Wokovu ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea: “Yule ambaye anaamini na kubatizwa ataokolewa; lakini yule ambaye haamini atahukumiwa” (Marko 16:16). “Kwa kuwa...

Njia ya Utakaso

Na Christopher, UfilipinoJina langu ni Christopher, na mimi ni mchungaji wa kanisa la nyumbani huko Ufilipino. Mnamo mwaka wa 1987,...

Kusadiki Uvumi Kunamaanisha Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho

Mafarisayo walieneza uongo na kumkashifu na kumkufuru Mungu, na sote tunaweza kukisia mwisho waliokumbana nao, lakini, je, wale watu wa Kiyahudi waliochukulia uongo na kashfa hizo kuwa ukweli—je, mwisho wao haukuwa wa huzuni hivyo? Walipitia maangamizi yasiyo ya kifani ya taifa na watu wa Kiyahudi walitawanyika pande zote. Hawakuwa na nyumbani pa kurudia kwa miaka 2,000. Je, haya siyo matokeo ya kuchukulia uongo wa Mafarisayo kuwa ukweli na kumpinga Mungu?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp