Nilipokuwa Mwenye Umri wa Miaka Kumi na Minane

12/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Pengine utayakumbuka maneno haya: ‘Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.’ Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. … Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki(Neno Laonekana katika Mwili). Kifungu hiki cha maneno ya Mungu kinanikumbusha nilipoteswa na CCP miaka michache iliyopita.

Karibu utusitusi siku moja mnamo Aprili 2017, nilikuwa katika mkutano na dada wengine wawili wakati ambapo zaidi ya dazeni ya maafisa wasio na sare rasmi waliingia ghafla. Kabla ya kuwa na wakati wa kujibu, maafisa kadhaa walitugandamiza chini, wakituambia tusisogee, huku wengine wakivuruga kila kitu, potepote. Haikuwachukua muda mrefu hata kidogo kuipetua nyumba hiyo. Tukio lililokuwa mbele yangu lilitisha. Moyo wangu ulikuwa ukipapa, na nilimwita Mungu tena na tena, “Ee Mungu! Naogopa sana, na sijui watatufanyia nini baadaye. Tafadhali nipe imani na nguvu ili niweze kuwa shahidi.” Nilikumbuka maneno haya ya Mungu baada ya maombi yangu: “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitegemeza imani na ujasiri wangu. Nilijua kwamba Mungu alikuwa nami, na bila kujali lile ambalo lingekuja, almradi nilimtegemea Mungu kwa dhati, Angekuwa nami. Nilipofikiria hayo, sikuhisi woga au hofu sana.

Wakati huohuo, afisa wa kike alinipiga kofi vikali mara kadhaa, kisha akafinya kidevu changu na kunipiga picha. Pia walitupekua, na wakachukua pesa na vitu vyetu vyote vya thamani. Baada ya hapo, walitupeleka sote watatu kwenye Ofisi ya Manispaa ya Usalama wa Umma ili tuhojiwe mmoja mmoja. Yule afisa aliyekuwa amenipiga picha alinifokea, “Wewe hufanya nini kanisani? Kiongozi wa kanisa ni nani? Toboa!” Wakati ambapo sikujibu, alifinya kidevu changu kwa ghadhabu kwa mkono wake wa kushoto na kukivuta juu kwa nguvu. Niliumizwa sana na jinsi alivyonifinya, nikilazimika kuchuchumia. Kisha aliinua mkono wake wa kulia kana kwamba alikuwa karibu kunigonga na akasema kwa tishio, “Hebu zungumza, vinginevyo tuna njia za kukushughulikia!” Kumwona akionekana mkatili sana kuliniacha nikiwa na hofu kidogo. Sikujua jinsi ambavyo angenitesa baadaye, kwa hivyo nilimwita Mungu upesi. Wakati huo maneno haya ya Mwenyezi Mungu yalinijia akilini: “Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu(Neno Laonekana katika Mwili). Niligundua kuwa mawazo yangu ya woga na ya kutisha yalitokana na udanganyifu wa Shetani, na kwamba polisi walitaka kuutesa mwili wangu ili kunifanya nimsaliti Mungu kwa sababu sikuweza kustahimili maumivu yale, na kuwasaliti ndugu zangu. Sikupaswa kulaghaiwa na hila za Shetani. Niliamua kwamba bila kujali jinsi polisi walivyonitesa, sitakuwa Yuda kamwe. Nilijua kwamba maisha na kifo changu vilikuwa mikononi mwa Mungu, na hawatanifanyia lolote bila ruhusa ya Mungu. Mara baada ya kugundua mambo haya nilihisi utulivu zaidi. Baada ya hapo, bila kujali alinifinya kidevu changu kwa nguvu jinsi gani huku akiniuliza mfululizo wa maswali, sikusema lolote. Wakati huo tu afisa mwingine alimwita aende zake, na mwishowe nikapumzika.

Karibu saa 9 alfajiri siku iliyofuata, nilipelekwa katika Kizuizi cha Manispaa. Pindi waliponitia ndani ya seli, afisa mmoja wa kike aliwaamuru wafungwa wengine wanivue nguo zote, kisha akanilazimisha niweke mikono yangu kichwani, nigeuke, na kufanya zoezi la kuchutama mbele ya kila mtu. Ilinibidi nifanye hivyo hadi waliporidhika, wakati ambapo wafungwa walisimama pembeni wakinizomea. Nilifadhaika na kuudhika sana wakati huo, na nilikuwa nikipiga kite tena na tena moyoni wangu, “Kwa nini mnanifedhehesha hivi?” Nisingepitia haya, nisingeamini kwamba hawa wanaodai kuwa “polisi wa umma” wanaweza kufanya kitu cha kustahili dharau kama hicho! Afisa huyo kisha aliwaambia wale wafungwa, “Anamwamini Mwenyezi Mungu, kwa hivyo yeye ni mlengwa wa hatua kali za serikali. Msikose kumfundisha sheria vizuri.” Kuanzia wakati huo, wafungwa wale walinitesa kila wakati na walinikaripia kwa kufanya lolote lile. Walinishurutisha nifanye kazi zote chafu zaidi na za kuchosha zaidi, kama vile kuosha vyombo, kufagia, na kusugua sakafu. Baada ya muda miguu yangu iliuma na nilichoka, lakini nilipopumzika kwa sekunde moja au kupunguza mwendo, walinifokea. Aidha, kila wakati ambapo sheria ya gereza ilivunjwa, walinilaumu. Sikuweza kabisa kujitetea kwa kutumia mantiki.

Kudhulumiwa na kutukanwa na wafungwa wengine mara nyingi kuliniacha nikihisi vibaya na dhaifu. Sikujua yote hayo yataisha lini, na usiku mwingi nilikunjamana chini ya blanketi yangu na kulia kimyakimya. Nilimwomba Mungu sana siku hizo. Nilipokuwa karibu kuchanganyikiwa, nilikumbuka maneno haya kutoka kwa Mungu: “Leo kila mtu atakuwa na majaribio machungu ya kukumbana nayo, vinginevyo moyo wa upendo ulio nao Kwangu hautakuwa wenye nguvu zaidi na hutakuwa na upendo wa kweli Kwangu. Hata kama majaribu haya yanajumuisha hali ndogo tu, kila mtu lazima ayapitie; ni kwamba tu ugumu wa majaribu utakuwa tofauti kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Majaribu ni Baraka kutoka Kwangu(Neno Laonekana katika Mwili). Nilielewa kwamba Mungu alikuwa Ameruhusu niwekwe katika hali hiyo na ilikuwa ili kukamilisha imani yangu na upendo wangu kwa Mungu ili nisimsaliti katika mazingira magumu kama hayo, na ili niweze kuwa shahidi na kumwaibisha Shetani. Nilikumbuka wakati ambapo kulikuwa na amani, nilikuwa nimejawa na imani, lakini sasa kwa kuwa nilikuwa nikipitia maumivu na aibu kiasi, nilikuwa dhaifu na hasi. Niliona jinsi ambavyo imani yangu katika Mungu haikutosha. Nilikuwa dhaifu sana, kama ua la nyumba ya kioo ya kuhifadhi mimea ambalo haliwezi kustahimili upepo na mvua kidogo. Kwa kupitia shida hizo, Mungu alikuwa Akikamilisha imani yangu na ilikuwa ya manufaa katika maisha yangu. Ilinibidi niwe shahidi na kumshuhudia Mungu.

Wiki moja baadaye, polisi walinipeleka kuhojiwa tena, na afisa mmoja alisema kwa unafiki, “Ukiwa mzuri na utuambie yote juu ya kanisa lako, tutakupigania ili uachiliwe kwa urahisi. Wewe ni mchanga sana, unapaswa kuwa kule nje ukifurahia ujana wako. Hufai kabisa kuwa hapa ukiteseka.” Afisa mwingine alisema, “Wanafunzi wenzako na marafiki zako wote wako kule nje wakifanya kazi ili kutimiza ndoto zao, huku wewe umefungwa kwa sababu unamwamini Mungu. Je, watakuwazia vipi wakijua?” Niliposikia wakisema haya, nilifikiria jinsi nilivyokuwa mchanga na sikustahili kuwa gerezani, na nilijiuliza iwapo marafiki na familia yangu watanicheka iwapo watajua. Kadiri nilivyozidi kufikiria hayo, ndivyo nilivyozidi kuchanganyikiwa, na kisha nikagundua kuwa sikuwa katika hali nzuri, kwa hivyo nilimwita Mungu haraka: “Ee Mungu, polisi wanaendelea kunisumbua. Sitaki kukusaliti na kuwa Yuda. Tafadhali linda moyo wangu, tafadhali niongoze ...” Kisha nilikumbuka kifungu hiki kutoka katika maneno ya Mungu: “Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani, … kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinikumbusha kwa wakati ufaao kwamba polisi walikuwa wadanganyifu katika mazungumzo yao kuhusu mustakabali wangu. Kwa kweli, walitaka tu kunipotosha, kunifanya nimsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu. Kwa kweli walikuwa waovu sana. Nilipofikiria hilo, nilisema kwa uthabiti, “Mimi ni mtu wa imani aliye kwenye njia ya kweli maishani. Bila kujali mnalosema, sitamsaliti Mungu.” Hilo liliwashtua maafisa wale. Hila yao haikuwa imefanikiwa, kwa hivyo upande wao mbaya ulitokeza mara moja. Mmoja aliniambia kwa kunitishia, “Inaonekana kwamba una mengi ya kusema kwa mtu mchanga sana kama wewe. Nakuambia, tunaweza kutafuta kisingizio chochote cha zamani cha kukufanya uhukumiwe miaka 8 au 10, au hata 15. Una umri wa miaka 18 sasa, kwa hivyo utatumia ujana wako wote gerezani!” Niliwaza, “Bila kujali nitahukumiwa miaka mingapi, nitamtegemea Mungu na kuwa shahidi. Sitakubali kumtii Shetani.”

Nilidhani kwamba walikuwa wametumia njia zao za vitisho na hongo na kwamba hawatanihoji tena. Sikuwahi kufikiria watajaribu kitu kiovu hata zaidi. Siku moja mwishoni mwa Mei, polisi walinipeleka katika chumba cha mahojiano na kusema, “Tulichunguza katika shule ya kaka yako mdogo na tukaona kwamba anafanya vizuri sana. Tuambie unachojua, kisha utaweza kwenda nyumbani mapema zaidi na kuungana na familia yako. Je, humkosi kaka yako?” Kusikia haya kuliniumiza. Mimi na kakangu tulikuwa wandani tangu tulipokuwa wadogo, lakini nilikuwa nikikimbia kwa miaka mingi ili kuepuka kukamatwa na CCP, na sikuweza kumuona. Sikujua alivyokuwa akiendelea. Walisema pia kwamba babangu alikuwa amerekodi video siku chache kabla, kisha wakaweka simu ya rununu mbele yangu na kuicheza video ile. Nilimwona baba yangu akiwa ameketi hapo akiwa hoi, nguo zake zikiwa zimekunjikunjika na akionekana mzee zaidi. Alisema kwenye kamera, “Xiaoyi, njoo nyumbani. Sote tumekukosa.” Polisi waliicheza mara kadhaa. Nilipokuwa nikimtazama babangu kwenye video hiyo, sikuweza kabisa kuacha kulia. Afisa mmoja alisema kwa kujipendekeza, “Hata kama hutajifikiria, unapaswa kuifikiria familia yako! Ikiwa umeazimia kumwamini Mungu, mbali na kutumikia kifungo, familia yako pia itahusishwa. Hata kaka yako akipita mitihani ya kuingia chuoni, hakuna shule itakayomchukua, na hataweza kupata kazi nzuri. Hata watoto wake wataingizwa lawamani. Ni bora ufikirie kwa uangalifu.” Kusikia hayo kulinifadhaisha sana. Nilimwomba Mungu bila kukoma: “Ee Mungu! Nimechanganyikiwa sana, na mimi ni dhaifu. Tafadhali linda moyo wangu ili nisifuate upendo wangu wa mwili, na niweze kushuhudia.” Nilikumbuka maneno haya ya Mungu baada ya maombi yangu: “Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinituliza polepole. Shetani alijua kwamba nilikuwa na hisia kali na sikuweza kuwaacha baba na kaka yangu, kwa hivyo alitumia hisia zangu na mustakabali wa familia yangu kunitishia, ili kunifanya nimsaliti Mungu na kuwa Yuda. Polisi walikuwa wenye kudhuru sana kwa siri! Kama ningemfuata Shetani na kumsaliti Mungu, hata kama ningeachiliwa na kuweza kuwa na familia yangu, ningejuta katika maisha yangu yote. Kisha nilifikiri juu ya jinsi ambavyo vitu vyote vimo mikononi mwa Mungu, kwa hivyo mustakabali wa kakangu utaamuliwa na kupangwa na Mungu. Pepo wa CCP hawakuwa na kauli ya mwisho. Kisha nilimwomba Mungu kimyakimya. Niliikabidhi familia yangu kwa utunzaji wa Mungu, na nikawa tayari kutii mipango Yake. Nilijibu, “Sina lolote la kusema!” Aliposikia hili, ofisa huyo aliiponda meza kwa hasira na kusema kwa sauti kuu, “Iwapo utakuwa mkaidi sana, usitulaumu kwa kuwa watovu wa adabu! Usifikirie kwamba hatuna hila zaidi katika mipango yetu ya siri. Kulingana tu na yale tuliyopata ulipokamatwa, tunaweza kuwakamata wazazi wako na kuwafanya wahukumiwe miaka mitatu hadi mitano, na kisha tuone jinsi kaka yako atakavyoishi peke yake nyumbani!” Kusikia haya kulinikasirisha sana. Mbali na CCP kutumia mbinu za kunitesa ili kunifanya nimsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu, pia walijaribu hata kunishurutisha kwa kutishia mustakabali wangu na ustawi wa familia. Nchini China, mtu anapomwamini Mungu, familia yake yote huteswa na CCP. Nilidharau kundi hilo la pepo na niliazimia kutoruhusu ujanja wao ufanikiwe. Kisha nilijibu kikaidi, “Naamini kuwa kila kitu kimo mikononi mwa Mungu. Hamtawahi kunifanya nimsaliti Mungu!” Afisa huyo aligonga meza ile tena kwa hasira, kisha akageuka na kuondoka kwa ghadhabu.

Asubuhi moja mwishoni mwa Mei, afisa wa kike alikuja na kuniachilia kutoka gerezani. Niliona kwamba hiyo ilikuwa ajabu sana. Kisha polisi walinipeleka katika kituo cha polisi cha eneo hilo. Nilipokuwa tu nikifikiri sana juu ya haya, niliwaona baba na babu yangu wakinitazama kwa matarajio huku polisi wakisimama pembeni, wakinitazama. Niligundua kwamba hawataniachilia kwa urahisi, lakini sikujua ni hila gani waliyokuwa wakijaribu kutumia. Mkuu wa kituo aliniambia baadaye, “Weka sahihi barua hii ya dhamana na tutakuacha uende nyumbani na uungane na familia yako.” Niliposoma hati hiyo, niliona kwamba ilisema: “Naahidi kutomwamini tena Mungu au kuwasiliana na washiriki wowote wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Sitafanya lolote kwa niaba ya kanisa, na sitachukua hati zozote za kwenda nje ya nchi katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Lazima pia niripoti kwa polisi mara nitakapopata notisi wakati wa dhamana ya mwaka mmoja.” CCP ilikuwa ikijaribu kunilazimisha nimsaliti Mungu na kuvunja uhusiano wote na kanisa. Nilikasirika sana, na nilikataa kabisa kuitia sahihi. Afisa mmoja alipoona jinsi nilivyokata shauri, alinitishia akisema, “Usipotia sahihi hati hii, utahukumiwa na kutumikia kifungo!” Baba na babu yangu waliingiwa na wasiwasi sana kwa sababu ya hilo na walinihimiza niharakishe kuitia sahihi. Walisema kwamba walikuwa wamelipa pesa kiasi na walikuwa wamejitahidi ili nipate dhamana huku nikisubiri uamuzi wa kesi, na kama ningeandika jina langu kwenye barua hiyo, ningeenda nyumbani. Hawakujua kabisa kwamba kutia sahihi kungemaanisha kuwa nilikuwa nikimkana na kumsaliti Mungu mbele ya Shetani, na kupoteza ushuhuda wangu. Nilianza kulia kutokana na shinikizo kubwa kutoka kwa polisi na familia yangu. Nilikuwa na msukosuko moyoni mwangu. Niliwaza, “Nisipotia sahihi, ni nani anayejua nitakuwa gerezani kwa muda gani. Lakini nikiitia sahihi, nitakuwa nikimsaliti Mungu!” Niliomba haraka moyoni mwangu na maneno haya kutoka kwa Mungu yalinijia akilini: “Natumai kwamba watu wote wanaweza kutoa ushuhuda wenye nguvu, unaovuma Kwangu mbele ya joka kubwa jekundu, kwamba waweze kujitolea wenyewe Kwangu kwa mara ya mwisho, na kutimiza matakwa Yangu kwa mara nyingine ya mwisho. Je, nyinyi mnaweza kufanya hili kweli?” (Neno Laonekana katika Mwili). Niliona haya nilipokabiliwa na matakwa ya Mungu. Bado nilikuwa nikizingatia mwili na mustakabali wangu badala ya kumridhisha Mungu. Nilitambua pia kwamba familia yangu kuniambia nitie sahihi barua ile na kukana imani yangu ilikuwa mojawapo ya hila za CCP. Imani yangu ilikuwa sahihi na inayostahiki, na nilikuwa kwenye njia sahihi maishani. Sikupaswa kuacha njia ya kweli na kumsaliti Mungu kwa sababu CCP ilinitishia na familia yangu ilinishinikiza. Niliamua kabisa kutoitia barua hiyo sahihi. Baada ya kufikiria hayo, nilisema kwa uthabiti, “Hamtawahi kunifanya niache imani yangu. Sahauni hilo!” Polisi walikasirika, lakini hawakuweza kufanya lolote. Mwishowe, walisema kwamba nitapata dhamana ya mwaka mmoja, na iwapo wangegundua kuwa nilikuwa nikiendelea kutenda imani yangu, wangenikamata na kuhakikisha kwamba nitapata hukumu kali.

Nilikwenda nyumbani, lakini CCP haikuwa imeniacha kabisa. Siku moja mwishoni mwa Juni mwaka wa 2017, polisi walimleta wakili mmoja nyumbani kwangu ili ajaribu kunitia kasumba. Alisema kwamba uhuru wa dini nchini China ulikuwa onyesho tu kwa wageni, na kwamba nchini China, tulilazimika kusikiliza Chama cha Kikomunisti. Alisema pia, “Chama kinaposema 'Ruka,' tunasema ‘Juu kiasi gani?', na Chama kikisema huwezi kuwa na imani, huwezi kuwa na imani. Vinginevyo, utapata kile unachostahili.” Hilo lilinighadhabisha. CCP hujaribu kila hila iliyopo kutufanya tuache imani yetu. Wakristo nchini China hawawezi kuishi kabisa! Nilikumbuka kifungu cha maneno ya Mungu ambacho ningependa kusoma pamoja na kila mtu. “Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! … Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu?(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno haya yatokayo kwa Mungu yalinisaidia kuona waziwazi kiini kiovu cha serikali ya CCP. CCP ni pepo wa Shetani ambaye huchukia ukweli na kumpinga Mungu. Kadiri ilivyozidi kunitesa vikali, ndivyo nilivyozidi kutaka kuiacha kabisa na kumfuata Mungu hadi mwisho! Polisi walikuja nyumbani kwangu mara kadhaa baadaye kunitia kasumba, na waliwafanya makada wa kijiji waniambie mara nyingi kwamba niiache imani yangu. Waliwafanya jamaa zangu pia waniambie niandike taarifa ya toba na kumsaliti Mungu. Kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, niliweza kushinda mashambulio na majaribu yote ambayo CCP ilinirushia na kuwa shahidi.

Hata ingawa niliteseka kidogo kimwili kutokana na kukamatwa kwangu na kuteswa na CCP, nilipata utambuzi ambao ulinifanya nione kiini kiovu cha CCP na uso wake wa pepo wa kumpinga Mungu. Niliiacha na kuikataa kwa dhati. Kupitia mateso na dhiki, maneno ya Mungu yaliniongoza kushinda hila za Shetani, na maneno Yake ndiyo yalinipa imani na nguvu ya kushinda udhaifu wangu wa mwili na kuwa shahidi. Kwa kweli nimejionea mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu na nina imani zaidi kuliko hapo awali ya kumfuata Mwenyezi Mungu!

Inayofuata: Kutoroka Hatari

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wakati wa mateso Ya Kikatili

Na Chen Hui, China Nililelewa katika familia ya kawaida nchini China. Baba yangu alikuwa katika jeshi na kwa sababu nilikuwa nimeongozwa na...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp