820 Ushuhuda Anaopaswa Kuwa Nao Mwanadamu

1 Kumshuhudia Mungu hasa ni suala la kuzungumza kuhusu maarifa yako ya kazi ya Mungu, kuhusu jinsi Mungu huwashinda watu, kuhusu jinsi Yeye huwaokoa watu, kuhusu jinsi Yeye huwabadili watu; ni suala la kuzungumza kuhusu jinsi Yeye huwaongoza watu kuingia katika uhalisi wa ukweli, Akiwawezesha washindwe, wakamilishwe na kuokolewa na Yeye. Kushuhudia kunamaanisha kuzungumza kuhusu kazi Yake na yote ambayo umepitia. Ni kazi Yake pekee inayoweza kumwakilisha, na ni kazi Yake pekee inayoweza kumfichua kwa umma, kwa ukamilifu Wake; kazi Yake inamshuhudia. Kazi na matamshi Yake vinamwakilisha Roho moja kwa moja. Vitu hivi vinaonyeshwa tu kupitia mwili wa Mungu, lakini kwa kweli, ni maonyesho ya Roho. Kazi yote Anayofanya na maneno yote Anayozungumza yanawakilisha kiini Chake. Kwa hivyo, unapomshuhudia Mungu, hushuhudii tu kuhusu sura Yake ya nje ya ubinadamu wa kawaida, lakini pia kazi Anayofanya na njia Anayoongoza; unapaswa kushuhudia kuhusu jinsi ulivyoshindwa na Yeye na umekamilishwa katika vipengele vipi. Unapaswa kuwa na ushuhuda wa aina hii.

2 Umepitia kuadibiwa, hukumu, usafishaji, majaribu, vipingamizi na majaribio hatua kwa hatua, na umeshindwa; umeweka kando matarajio ya mwili, nia zako binafsi, na maslahi ya ndani ya mwili. Yaani, maneno ya Mungu yameushinda moyo wako kabisa. Ingawa hujakua katika maisha yako kwa kiwango Anachotaka, unayajua mambo haya yote na unashawishika kabisa na kile Anachofanya. Kwa hivyo, hili linaweza kuitwa ushuhuda, ushuhuda ambao ni halisi na wa kweli. Kazi ambayo Mungu amekuja kufanya, kazi ya hukumu na kuadibu, inakusudiwa kumshinda mwanadamu, lakini pia Anahitimisha kazi Yake, akimaliza enzi na kutekeleza kazi ya hitimisho. Anakamilisha enzi nzima, Akiwaokoa wanadamu wote, Akiwakomboa wanadamu kutoka katika dhambi kabisa; Anawapata wanadamu Aliowaomba kikamilifu. Unapaswa kushuhudia haya yote. Katika siku zijazo, wakati injili inaenezwa, unapaswa kuweza kuzungumzia maarifa yako mwenyewe, ushuhudie yote uliyoyapata moyoni mwako na utumie jitihada yote. Kiumbe aliyeumbwa anapaswa kufanikisha hili.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 819 Unajua Kusudi na Maana ya Kazi ya Mungu?

Inayofuata: 821 Jinsi ya Kumshuhudia Mungu Katika Imani Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp