Sura ya 40

Watu hukodolea macho kila mwendo Wangu, kana kwamba Nakaribia kuleta mbingu chini, na wao kila mara hukanganyikiwa na shughuli Zangu, kana kwamba matendo Yangu ni yasiyoeleweka kabisa kwao. Hivyo, wao hufuata nyayo Zangu kwa yote watendayo, wakiogopa sana kwamba watakosea Mbinguni na kutupwa katika “ulimwengu wa wenye kufa.” Sijaribu kuwashikilia watu, ama Huufanya upungufu wao lengo la kazi Yangu. Wakati huu, wanafurahia sana, na kuja kunitegemea Mimi. Ninapotoa kwa mwanadamu, watu hunipenda Mimi jinsi wayapendavyo maisha yao wenyewe, lakini Niulizapo vitu kutoka kwao, wao hujitenga na Mimi. Ni kwa nini? Hawawezi hata kutia katika matendo “haki na akili” ya ulimwengu wa mwanadamu? Kwa nini Natoa matakwa kama hayo kwa watu tena na tena? Je, ni kweli kwamba Sina chochote? Watu hunichukulia Mimi kama mwombaji. Niombapo vitu kutoka kwao, wao hushikilia “makombo” yao mbele Yangu ili “Niyafurahie,” na hata husema wananitunza Mimi kwa njia maalum. Mimi huziangalia sura zao mbaya na vioja, na Mimi huondoka kwa mwanadamu tena. Chini ya hali kama hizi, watu husalia wasiofahamu, na huchukua tena vitu Nilivyowanyima, wakingoja kurudi Kwangu. Nimetumia wakati mwingi, na kulipa gharama kubwa, kwa ajili ya mwanadamu—lakini wakati huu, kwa sababu isiyojulikana, dhamiri za watu zimesalia zisizoweza kamwe kutekeleza shughuli zao za asili. Kutokana na hilo, Naorodhesha tashwishi zao za kuendelea kati ya “maneno ya fumbo,” kutumika kama “rejeleo” la vizazi vya baadaye, kwa sababu haya ni “matokeo ya uchunguzi wa kisayansi” yaliyozaliwa na “kazi ngumu” ya watu; Ningeyaondoaje kwa kawaida? Hii haingekuwa “kusikitisha” makusudi mazuri ya watu? Kwani Mimi, hata hivyo, Nina dhamiri, Sijishughulishi na mwanadamu katika matendo ya ujanja, ya kutapeli—je, matendo Yangu siyo hivyo? Je, hii siyo “haki na akili” inayozungumziwa na mwanadamu? Miongoni mwa binadamu, Nimefanya kazi bila kukoma mpaka wakati wa sasa. Na kuwasili kwa nyakati kama leo, watu bado hawanijui Mimi, wao bado hunichukulia Mimi kama mgeni, na hata, kwa kuwa Nimewapeleka “ukingoni” wao hukuza chuki zaidi Kwangu. Wakati huu, upendo katika mioyo yao umetoweka kitambo bila dalili. Sijisifu, seuze kumdunisha mwanadamu. Naweza kumpenda mwanadamu milele, na pia Naweza kumchukia milele, na hili kamwe halitabadilika, kwani Nina ustahamilivu. Lakini mwanadamu hana ustahamilivu huu, yeye kila mara hughairighairi Kwangu, yeye kila mara hunisikiliza kidogo tu Nifunguapo kinywa Changu, na Nifungapo kinywa Changu na kutosema chochote, yeye punde hupotea kati ya mawimbi ya ulimwengu mkubwa. Hivyo, Mimi hufupisha hili katika methali nyingine: Watu hukosa ustahimilivu, na hivyo hawawezi kuutimiza moyo Wangu.

Huku watu wanapoota, Nasafiri katika nchi za dunia Nikinyunyizia “harufu ya kifo” iliyo mikononi Mwangu miongoni mwa binadamu. Watu wote ghafula huacha uchangamfu na kuingia katika daraja inayofuata ya maisha ya binadamu. Miongoni mwa wanadamu, viumbe vinavyoishi haviwezi kuonekana tena, maiti imetapakaa kila mahali, vitu vinavyojawa na uchangamfu hutoweka mara moja bila dalili, na harufu ya kusonga ya maiti huenea kote ardhini. Mimi huufunika uso Wangu mara moja na kuondoka kwa mwanadamu, kwa kuwa Naanza hatua inayofuata ya kazi, kuwapa wale ambao wamekuwa hai mahali pa kuishi na kusababisha watu wote kuishi katika nchi iliyo bora. Hii ni nchi iliyobarikiwa—nchi isiyo na huzuni au kuhema kwa majonzi—Niliyomtayarishia mwanadamu. Maji yabubujikayo kutoka kwa chemchemi za bonde ni safi kabisa, meupe kabisa ya kuweza kuonekana mpaka chini, yanatiririka bila kukoma na kamwe hayakauki, watu huishi kwa upatanifu na Mungu, ndege huimba, na kati ya upepo mwanana na jua la vuguvugu, mbingu na dunia vyote ni tulivu. Leo, hapa, maiti ya watu wote imelala hapa na pale katika mchafukoge. Bila watu kujua, Naachilia ndwele yoyote yenye kufisha iliyo mikononi Mwangu, na miili ya binadamu huoza, bila kuacha dalili yoyote ya mwili kutoka utosini hadi kidoleni, na Naenda mbali sana kutoka kwa mwanadamu. Kamwe Sitakusanyika na mwanadamu tena, kamwe Sitakuja miongoni mwa binadamu, kwani hatua ya mwisho ya usimamizi Wangu wote imefika mwisho, na Sitawaumba wanadamu tena, Sitatilia maanani mwanadamu tena. Baada ya kusoma maneno kutoka kinywani Mwangu, watu wote hukosa tumaini, kwani hawataki kufa—lakini ni nani “hafi” kwa ajili ya “kuwa hai”? Ninapowaambia watu Nakosa mazingaombwe ya kuwafanya kuwa hai, wao huangua kilio kwa uchungu; kweli, ingawa Mimi ndiye Muumba, Ninayo tu nguvu ya kuwafanya watu wafe, na Nakosa uwezo wa kuwafanya wawe hai. Kwa hili, Naomba msamaha kwa mwanadamu. Hivyo, Nilimwambia mwanadamu kabla kwamba “Nina deni lake lisilolipika”—lakini alidhani Nilikuwa nakuwa mpole. Leo, na majilio ya ukweli, bado Nasema hili. Sitausaliti ukweli Ninenapo. Katika dhana zao, watu huamini kwamba kuna njia nyingi ambazo kwazo Mimi huzungumza, kwa hiyo wao kila mara hukamata imara maneno Ninayowapa huku wakitumaini kitu kingine. Je, hizi sizo motisha zenye kosa za mwanadamu? Ni chini ya hali hizi ndiyo Nathubutu kusema “kwa ujasiri” kwamba mwanadamu hanipendi kweli. Singekana dhamiri na kupotosha ukweli, kwa kuwa Singewapeleka watu katika nchi yao iliyo bora; mwishowe, wakati ambapo kazi Yangu itaisha, Nitawaongoza katika nchi ya kifo. Kwa hiyo ni bora kabisa watu wasilalamike kunihusu—je, sio kwa sababu watu “hunipenda” Mimi? Je, sio kwa sababu shauku yao ya baraka ni ya nguvu sana? Kama watu hawangetaka kutafuta baraka, kungekuwaje na “msiba” huu? Kwa ajili ya “uaminifu” wa watu Kwangu, kwa vile wamenifuata Mimi kwa miaka mingi, wakifanya kazi kwa bidii licha ya kutotoa mchango wowote kamwe, Nawafichulia machache ya kile kinachofanyika katika chumba cha siri. Kwa vile, leo, kazi Yangu bado haijafikia kiwango fulani na watu bado hawajatupwa katika shimo la moto, Nawashauri waondoke mara wanapoweza—wote ambao watabaki wataelekea kupitia msiba na bahati kidogo, na bado hawataweza kuepuka kifo mwishowe. Nawafungulia wazi “milango ya utajiri”; yeyote ambaye yuko radhi kuondoka aanze safari mara anapoweza—kama atangoja mpaka kuadibu kufike, atakuwa amechelewa sana. Maneno haya si dhihaka—ni ukweli halisi. Maneno Yangu yanatamkwa kwa mwanadamu kwa dhamiri nzuri, na kama hamtaenda sasa, mtaenda lini? Watu kweli wanaweza kuyaamini maneno Yangu?

Sijawahi kufikiria sana kuhusu majaliwa ya mwanadamu; Mimi hufuata tu mapenzi Yangu mwenyewe, Sizuiliwi na watu. Ningeondoaje mkono Wangu kwa sababu ya woga wao? Kotekote katika mpango wa usimamizi Wangu wote, Sijawahi kamwe kufanya matayarisho zaidi kwa ajili ya matukio ya mwanadamu. Mimi hutenda tu kwa kadri ya mpango Wangu wa asili. Zamani, watu “walijitolea” wenyewe Kwangu na Sikuwa moto wala baridi kwao. Leo, wamejitoa wenyewe “sadaka” Kwangu, na Naendelea kutokuwa moto wala baridi kwao. Sijaridhika kwa sababu watu wanatoa sadaka ya maisha yao kwa ajili Yangu, wala Sijawi na furaha nyingi, bali Naendelea kuwapeleka katika eneo la uangamizi kwa mujibu wa mpango Wangu. Sitilii maanani mtazamo wao wakati wa kukiri—Moyo Wangu usio kunjufu, wa baridi ungewezaje kuguswa na mioyo ya binadamu? Je, Mimi ni mojawapo wa wanyama wenye mhemko miongoni mwa wanadamu? Mara nyingi Nimewakumbusha watu kwamba Mimi sina hisia, lakini wao hutabasamu tu, wakiamini Nakuwa mpole tu. Nimesema kwamba “Mimi sijui falsafa za maisha za ulimwengu wa mwanadamu,” lakini watu hawajawahi kufikiria hivyo, na wakasema kwamba njia ambazo kwazo Mimi hunena ni nyingi sana. Kwa sababu ya vizuizi vya dhana hii ya mwanadamu, Sijui ni kwa toni gani, na kwa njia gani, kunena na watu—na kwa hiyo, bila chaguo lingine, Naweza tu kuzungumza waziwazi na toni ya kuwaambia. Naweza kufanya nini kingine? Njia ambazo kwazo watu huzungumza ni nyingi sana—wao husema “Sitegemei hisia bali Natenda haki,” ambayo ni aina ya wito wametangaza kwa miaka mingi, lakini hawawezi kutenda kwa mujibu wa maneno yao, maneno yao ni matupu—kwa hiyo Nasema kwamba watu hukosa uwezo kwani “maneno yao na utimilifu hutokea sawia.” Ndani ya mioyo yao, watu huamini kwamba kutenda hivyo ni kuniiga Mimi—lakini Sina haja ya uigaji wao, Nimechoshwa nao. Kwa nini watu kila mara humpinga Yule ambaye huwalisha? Je, Nimempa mwanadamu kidogo sana? Kwa nini watu kila mara humwabudu Shetani kisirisiri bila Mimi kujua? Ni kana kwamba wao hunifanyia Mimi kazi na mshahara wa kila mwezi ambao Mimi huwapa hautoshi kukidhi gharama ya maisha yao, kwa sababu hiyo wao hutafuta kazi nyingine nje ya saa za kufanya kazi ili waweze kuzidisha mara mbili ujira wao—kwani matumizi ya watu ni makubwa sana, na inaonekana hawajui namna ya kuendelea kuishi. Kama kweli ingekuwa hivyo, Ningewaambia waondoke katika “kiwanda” Changu. Zamani sana Nilimweleza mwanadamu kwamba kunifanyia Mimi kazi hakuhusishi utendewaji maalum: Bila kinzano, Mimi huwatendea watu kwa haki na kwa kweli, kwa kuchukua mfumo wa “fanya bidii pata zaidi, fanya kidogo pata kidogo, usifanye kazi yoyote hutapata chochote.” Nizungumzapo, Sifichi chochote; kama yeyote anaamini “sheria za kiwanda” Changu kuwa kali mno, anatakiwa kuondoka mara moja, Nitalipia “gharama ya usafiri” wao. Mimi ni “mwenye huruma” katika kuwashughulikia watu kama hao, Siwalazimishi kubaki. Kati ya watu hawa wasiohesabika, Singempata “mfanyakazi” ambaye anaupendeza moyo Wangu mwenyewe? Watu hawapaswi kunidharau Mimi! Kama watu bado wananiasi Mimi na watake kutafuta “ajira” mahali pengine, Sitawalazimisha—Ningelikaribisha, Sina budi! Je, sio kwa sababu Nina “sheria na kanuni” nyingi mno?

Mei 8, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 39

Inayofuata: Sura ya 41

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp