582 Ni Waaminifu Tu Ndio Wanaoweza Kutekeleza Wajibu Wao kwa Kuridhisha

1 Unapokuwa ukitimiza wajibu wako, unapaswa kujichunguza kila wakati ili uone iwapo unafanya mambo kulingana na kanuni, iwapo utendaji wa wajibu wako unafikia kiwango kinachotakiwa, iwapo unaufanya tu kwa uzembe au la, iwapo umejaribu kukwepa majukumu yako na iwapo kuna matatizo yoyote katika mtazamo wako na jinsi unavyofikiri. Mara baada ya kutafakari juu yako mwenyewe na kuelewa kabisa mambo haya, utatimiza wajibu wako kwa urahisi zaidi. Bila kujali unakabiliwa na nini unapokuwa ukifanya wajibu wako—uhasi na udhaifu, au kuwa katika hali mbaya baada ya kushughuliwa—unapaswa kuuchukulia vizuri, na lazima pia utafute ukweli na uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa kufanya mambo haya, utakuwa na njia ya kutenda.

2 Iwapo ungependa kutimiza wajibu wako vizuri, basi sharti usiathiriwe na hali yako ya moyo. Bila kujali unahisi kwamba wewe ni hasi au dhaifu jinsi gani, unapaswa kutenda ukweli katika kila kitu unachofanya, kwa ukamilifu kabisa na kwa kufuata kanuni. Ukifanya hivi, mbali na watu wengine kukupenda, Mungu pia atakupenda. Hasa, utakuwa mtu mwaminifu na anayewajibika; utakuwa mtu mzuri kwa kweli ambaye hutimiza wajibu wake kufikia kiwango kinachotakiwa na anayeishi kwa kudhihirisha kikamilifu mfano wa mtu halisi. Watu kama hao hutakaswa na hufanikisha mabadiliko ya kweli wanapotimiza wajibu wao, na wanaweza kusemekana kuwa waaminifu machoni pa Mungu. Watu waaminifu pekee ndio wanaoweza kuvumilia kutenda ukweli na kufanikiwa katika kutenda kwa maadili, na wanaweza kutekeleza wajibu wao kufikia kiwango kinachotakiwa.

Umetoholewa kutoka katika “Uingiaji Katika Uzima Lazima Uanze na Uzoefu wa Kutenda Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 581 Ni kwa Kutenda kwa Maadili Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kufanya Wajibu Wake Vyema

Inayofuata: 583 Kuwa Mtu Anayemridhisha Mungu na Kutuliza Akili Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp