Njia … (2)

Labda ndugu zetu wana muhtasari kidogo wa utaratibu, hatua, na mbinu za kazi ya Mungu katika China bara, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba ni heri kuwa na kumbukumbu au muhtasari kidogo wa ndugu zetu. Ninatumia tu nafasi hii kusema machache ya kile kilicho moyoni Mwangu; Sizungumzi juu ya chochote nje ya kazi hii. Natarajia kwamba ndugu wanaweza kuelewa hali ya moyo Wangu, na pia Naomba kwa unyenyekevu kwamba wote wanaosoma maneno Yangu wafahamu na kusamehe kimo Changu kidogo, kwamba uzoefu Wangu wa maisha kweli si wa kutosha, na kwamba kweli Siwezi kuwa na ujasiri mbele ya Mungu. Kwa hali yoyote, Mimi huhisi kila mara kwamba hizi ni sababu halisi tu. Kwa kifupi, lolote litokealo, hakuna watu, matukio, au vitu vinavyoweza kuzuia ushirika wetu machoni pa Mungu, na Natarajia kwamba ndugu zetu wanaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi mbele ya Mungu pamoja na Mimi. Ningependa kuomba ombi lifuatalo: “Ee Mungu! Tafadhali tuonyeshe fadhili ili Mimi na ndugu Zangu tuweze kujitahidi pamoja chini ya utawala wa maadili yetu ya pamoja, tuwe waaminifu Kwako hadi kifo, na tusiwahi kuvunja ahadi hii!” Maneno haya ni azimio Nililoweka mbele ya Mungu, lakini ingeweza pia kusemwa kwamba ni wito Wangu kama mwanadamu wa mwili anayetumiwa na Mungu. Nimeeleza hili mara nyingi katika ushirika pamoja na ndugu walio kandokando Yangu, na Nimetoa hili kama ujumbe kwa wale walio ubavuni Mwangu. Sijui watu wanalifikiria vipi, lakini bila kujali lolote litokealo, Naamini kwamba hawana tu hali ya juhudi za dhahania, lakini hata zaidi, pia wana hali ya nadharia halisi. Kwa sababu ya hili, inawezekana kwamba watu wengine wana maoni fulani, na unaweza kuyachukua maneno haya kama wito wako na kuona jinsi msukumo wako wa kumpenda Mungu utakavyokuwa mkuu. Watu wengine watakuza fikira fulani watakaposoma maneno haya, na kufikiria: “Ni jinsi gani jambo hili la kusema kila siku, la kawaida linaweza kuwapa watu msukumo mkuu wa kumpenda Mungu hadi kifo? Na halina uhusiano wowote na mada ya kile tunachojadili, ‘Njia.’” Nakubali kwamba maneno haya hayana kiwango kikubwa sana cha uzuri, lakini Nimefikiria kila mara kwamba yanaweza kuwaongoza watu katika njia sahihi, na kuwaruhusu kupitia aina zote za majaribu kwa mwelekeo wa njia ya imani katika Mungu bila kukata tamaa au kurudi nyuma. Hii ndiyo maana kila mara Nauchukulia huu kuwa wito Wangu, na Natarajia kwamba watu wanaweza kufikiria juu ya hili kwa makini. Hata hivyo kusudi Langu si kumlazimisha kila mtu kukubali maoni Yangu—hili ni pendekezo tu. Bila kujali kile ambacho watu wengine wanafikiria kunihusu Mimi, Nafikiri kwamba Mungu atafahamu uwezo wa ndani wa kila mmoja wetu. Mungu daima anafanya kazi juu ya kila mmoja wetu, na kazi Yake ni isiyochoka. Hii ni kwa sababu sote tulizaliwa katika nchi ya joka kuu jekundu—hii ndiyo maana Anafanya kazi kwa njia hii ndani yetu. Wale waliozaliwa katika nchi ya joka kuu jekundu wana bahati kupata aina hii ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kama mmoja wao, Nahisi sana pendo, heshima, pamoja na kupendeza kwa Mungu. Huyu ni Mungu anayetutunza. Ufalme ulio nyuma kimaendeleo, wenye kushikilia ukale, wa kikabaila, wa ushirikina, na wa upotovu wa tabaka la wafanyakazi kama huu hupata aina hii ya kazi kutoka kwa Mungu. Kutokana na hili, ni wazi kwamba sisi, kundi hili la watu katika enzi ya mwisho, tumebarikiwa sana. Naamini kwamba ndugu wote ambao macho yao ya kiroho yamefunguka kuiona kazi hii watalia machozi ya furaha kama matokeo. Na wakati huo, je, hutajionyesha kwa Mungu kwa kucheza na furaha? Je, hutamtolea Mungu wimbo ulio moyoni mwako? Wakati huo, je, hutaonyesha azimio lako kwa Mungu na kufanya mpango mwingine mbele Yake? Nafikiri kwamba yote haya ni mambo ambayo watu wa kawaida wanoamwamini Mungu wanapaswa kufanya. Kama wanadamu, Naamini kwamba kila mmoja wetu anapaswa kuwa na aina fulani ya maonyesho mbele ya Mungu. Hili ndilo mtu aliye na hisia anapaswa kufanya. Kwa kutazama uhodari wa kila mmoja miongoni mwetu na vilevile mahali petu pa kuzaliwa, inaonyesha kiwango cha aibu ambayo Mungu alivumilia ili kuja miongoni mwetu. Ingawa tuna maarifa fulani ya Mungu ndani yetu, kulingana na kile tunachojua, Mungu ni mkuu sana, mwenye uwezo mkubwa kabisa, na wa heshima sana, inatosha kujua jinsi mateso Yake yamekuwa makubwa miongoni mwa wanadamu kwa ulinganishi. Lakini hili bado ni jambo lisilo dhahiri kusema, na watu wanaweza tu kulichukulia kama maneno na mafundisho ya dini. Hii ni kwa sababu wale walio miongoni mwetu ni wasiosikia na wenye akili goigoi. Naweza tu kuongeza juhudi katika kueleza suala hili kwa wale ndugu wote ambao wangelikubali ili roho zetu ziweze kusisimuliwa na Roho wa Mungu. Mungu afungue macho yetu ya kiroho ili tuweze kuona gharama ambayo Mungu amelipa, juhudi ambazo Amefanya, na nguvu ambazo Ametumia kwa ajili yetu.

Kama mmoja wa wale walio katika China bara ambaye amekubali Roho wa Mungu, Nahisi kwa kina kwamba uhodari wetu unakosekana kweli. (Natarajia kwamba ndugu zetu hawatahisi vibaya kwa sababu ya hili—huu ni uhalisi wa hali.) Katika maisha Yangu ya utendaji Nimeona kwa dhahiri kwamba kile tunacho na tulicho yote ni yaliyo nyuma sana kimaendeleo. Katika hali kuu, ni jinsi tunavyotenda katika maisha yetu na uhusiano wetu na Mungu, na katika hali ndogo, ni kila wazo na fikira. Hivi vyote ni vitu vinavyoishi kwa uhalisi na ni vigumu kuficha kwa maneno au vitu vya uongo. Kwa hivyo, Nisemapo hili watu wengi huashiria kwa vichwa vyao na kulikubali, na wao huridhishwa nalo isipokuwa wawe ni watu wanaokosa mantiki ya kawaida. Mtu wa aina hiyo hawezi kukubali aina hii ya mtazamo Wangu. Labda sijui kwa kweli jinsi ya kuwa wa adabu, na Ninamtaja kwa waziwazi mtu wa aina hiyo kama mnyama kwa hakika. Hii ni kwa sababu mtu wa aina hiyo ni wa chini sana juu ya mti wa mzimu katika nchi ya joka kuu jekundu—yeye ni kama nguruwe au mbwa. Mtu wa aina hiyo amepungukiwa sana katika uhodari, na hastahili kuja mbele ya Mungu. Labda ni kwamba maneno Yangu ni ya kifidhuli sana. Kwa kumwakilisha Roho wa Mungu anayefanya kazi ndani Yangu, Mimi nalaani aina hii ya kiumbe aliye kama mnyama, mchafu, na Natarajia kwamba ndugu Zangu hawadhoofishwi na hili. Inawezekana kwamba hatuna mtu wa aina hii miongoni mwetu, lakini bila kujali ukweli ni upi, Naamini kwamba hivi ndivyo mtu wa aina hiyo anapaswa kushughulikiwa. Unaonaje?

Miaka elfu kadhaa ya ufalme wa joka kuu jekundu umepotoshwa wakati huo wote mpaka sasa, na kwa sababu umempinga Mungu kwa uthabiti, Mungu ameilaani nchi hii na kuishughulikia kwa ghadhabu, na baada ya hilo Ameigawia kuadibu Kwake. Nchi hii iliyolaaniwa na Mungu imetawaliwa na utenganisho wa kimbari, na bado iko katika hali ya kuwa nyuma kimaendeleo. Nchi tuliyozaliwa ndani ni uwanja wa mkusanyiko wa pepo wabaya wengi, na kwa hivyo wanatapakaa kote na kutafuta kutawala katika nchi hii. Hili limesababisha kuchafuliwa kwa wale waliozaliwa hapa. Mienendo, mila, na mawazo na dhana za watu ni za nyuma kimaendeleo na za mtindo wa zamani, kwa hiyo zinaunda aina zote za fikira kuhusu Mungu ambazo kufikia sasa wameshindwa kuziondoa. Hasa, wao hutenda kwa njia moja mbele ya Mungu na kutenda kwa njia nyingine nyuma Yake, wakidhania kumhifadhi Shetani ni kumhudumia Mungu. Hili ni onyesho la kuwa nyuma sana kimaendeleo. Mungu amefanya kazi nyingi sana katika China bara na Amenena maneno Yake mengi sana, lakini watu bado ni wasiosikia kabisa na wasiojali. Bado wanafanya kazi yao kama walivyofanya awali na hawana kabisa ufahamu wa maneno ya Mungu. Mungu alipotangaza kwamba hakukuwa na mategemeo na wala matumaini, kanisa lililokuwa hai na lenye joto la majira ya joto liliingia katika majira ya baridi. Nafsi halisi za watu zilifichuliwa katika nuru ya mchana na ujasiri, upendo, na nguvu zao za awali vyote vilitoweka bila dalili yoyote. Na sasa, hakuna aliyepata tena uchangamfu wake. Wanasema na maneno yao kwamba wanampenda Mungu, na ingawa hawathubutu kulalamika katika mioyo yao, haijalishi chochote hawana upendo huo katu. Hilo linahusu nini? Nafikiri kwamba ndugu zetu wataukubali ukweli huu. Mungu atupe nuru, ili sote tuweze kujua kupendeza Kwake, kumpenda Mungu wetu katika kina cha mioyo yetu, na kuonyesha upendo ambao sote tunao kwa Mungu katika nafasi mbalimbali; Mungu atupe mioyo thabiti yenye upendo wa kweli Kwake—hili ndilo Ninalotarajia. Baada ya kusema hili, Nahisi huruma kidogo kwa ndugu Zangu waliozaliwa pia katika nchi hii ya uchafu, na kwa hiyo chuki yangu dhidi ya joka kuu jekundu imekua ndani yangu. Linazuia upendo wetu kwa Mungu na kushawishi ulafi wetu wa matazamio yetu ya baadaye. Linatushawishi kuwa wabaya, kumpinga Mungu. Limekuwa joka kuu jekundu ambalo limetudanganya, limetupotosha, na kutuangamiza mpaka sasa, kiasi kwamba hatuwezi kulipa upendo wa Mungu kwa mioyo yetu. Tuna msukumo ndani ya mioyo yetu lakini ijapokuwa sisi wenyewe, hatuna nguvu. Sisi sote ni waathiriwa. Kwa sababu hii, Nalichukia kutoka kwa kiini Changu na Siwezi kungoja kuliharibu. Kwa hali yoyote, Ninapofikiria tena, hili halingekuwa na mafanikio na lingeleta tu tatizo kwa Mungu, kwa hiyo Narudi kwa maneno haya—Nimeamua kuyafanya Mapenzi Yake—kumpenda Mungu. Hii ndio njia Ninayofuata—ni njia ambayo Mimi, mmoja wa viumbe Wake, Napaswa kuitembea. Ni jinsi Napaswa kuishi maisha Yangu. Haya ni maneno kutoka moyoni Mwangu, na Natarajia kwamba ndugu Zangu watapata kutiwa moyo kwa kiasi fulani baada ya kuyasoma maneno haya ili moyo Wangu uweze kupata kiasi fulani cha amani. Kwa kuwa lengo Langu ni kuyafanya mapenzi ya Mungu na hivyo kuishi kwa kudhihirisha maisha yaliyojaa maana na mng’aro. Katika hili, Nitaweza kufa bila majuto, na moyo uliojaa furaha na faraja. Je, ungependa kufanya hilo? Wewe ni mtu aliye na aina hiyo ya azimio?

Kwamba Mungu anaweza kufanya kazi ndani ya wale wanaoitwa “Mtu Mgonjwa wa Asia Mashariki” ni nguvu Zake kuu. Ni unyenyekevu na kujificha Kwake. Bila kujali maneno Yake makali au kuadibu kunakoelekezwa kwetu, tunapaswa kumsifu Yeye kutoka ndani ya mioyo yetu kwa unyenyekevu Wake, na kumpenda Yeye mpaka mwisho kabisa wa hili. Watu ambao wamefungwa na Shetani kwa miaka elfu kadhaa wameendelea kuishi chini ya ushawishi wake na hawajamtupilia mbali. Wameendelea kupapasa na kupambana kwa uchungu. Zamani wangefukiza, na kumwinamia na kumhifadhi Shetani, na walikuwa wamefungwa kabisa kwa mitego ya familia na ya kidunia pamoja na maingiliano ya kijamii. Hawakuweza kuyatupilia mbali. Katika aina hii ya jamii ya unyang’au, ni wapi ambapo mtu anaweza kupata maisha ya maana? Kile ambacho watu husimulia ni maisha ya mateso, na kwa bahati nzuri, Mungu amewaokoa watu hawa wasio na hatia, na kuyaweka maisha yetu chini ya utunzaji Wake na ulinzi Wake ili maisha yetu yawe ya furaha na yasiyojaa tena wasiwasi. Tumeendelea kuishi chini ya neema Yake mpaka sasa. Je, hii si baraka ya Mungu? Mtu anawezaje kuthubutu kumdai Mungu kupita kiasi? Ametupa chache sana? Bado hamjaridhika? Nafikiri kuwa wakati umewadia wa sisi kulipa upendo wa Mungu. Ingawa tutapata mara kwa mara dhihaka, kashfa, na mateso mengi sana kwa sababu tunafuata njia ya imani katika Mungu, Naamini hili ni jambo la maana. Ni jambo la utukufu, sio aibu, na lolote litokealo, baraka tunazofurahia si hafifu kamwe. Katika nyakati nyingi za masikitiko, maneno ya Mungu yameleta faraja, na kufumba na kufumbua, huzuni imegeuka na kuwa furaha. Katika nyakati nyingi za hitaji, Mungu ameleta baraka na tumekimiwa kupitia kwa maneno Yake. Katika nyakati nyingi za magonjwa, maneno ya Mungu yameleta uzima—tumewekwa huru kutoka kwa hatari, na kugeuka kutoka kwa hatari hadi kwa usalama. Tayari umefurahia vitu vingi kama hivi bila kutambua hilo. Inawezekana kwamba hukumbuki?

Iliyotangulia: Njia … (1)

Inayofuata: Njia … (3)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp