Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho Chaguzi

Yaliyomo

Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili Ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mimi hueneza kazi Yangu katika mataifa. Katika ulimwengu mzima unang’aa utukufu Wangu; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi Ninayosambaza. Kuanzia sasa, Ninaingia enzi mpya na kuleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Ninaporudi katika "nchi Yangu," Ninaanza sehemu nyingine ya kazi katika mpango Wangu wa awali ili mwanadamu aje kujua zaidi kunihusu. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, hivyo Mimi Nasafiri huku na kule kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Ni enzi mpya, licha ya yote, na Ninaleta kazi mpya ili niwachukue watu wapya zaidi katika enzi mpya na kuwatupa kando zaidi ya wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Ninatekeleza hatua ya kazi isiyoweza kueleweka na mwanadamu na kuwafanya kutingika katika upepo, ambapo baadaye wengi kwa kimya watabebwa na upepo unaovuma. Huu ni "uwanja wa kupura" Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu kwa kimya wameingia ndani wakati wa kazi Yangu, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakapokuwa chemchemi ya uzima, ili wale wanaonipenda watapata kutoka Kwangu matunda ya mtini na harufu ya maua. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi, ila ni mchanga tu. Kwa sababu ya kukabiliwa na hili, Ninafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni safi, dhahabu safi, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea katika Paradiso Yangu? Ninatumia kila mbinu linaloweza kuwazwa kuwafukuza. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Kuchukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wao wanalazimika kuondoka Kwangu. Hili ndilo Mimi huwawafanyia waovu, lakini bado kuna siku ya wao kufanya huduma Kwangu. Hamu ya watu kupata baraka ni nyingi mno; Kwa hivyo Ninageuza mwili Wangu na kuonyesha uso Wangu wa utukufu kwa mataifa ili watu wote waishi katika dunia yao wenyewe na kujihukumu, Ninaposema maneno ambayo ni lazima Niyaseme na kuwasambazia binadamu wanachohitaji. Wakati wanadamu wanapopata fahamu, Nitakuwa kwa muda mrefu Nimeeneza kazi Yangu. Kisha Nitawaeleza wanadamu mapenzi Yangu, na kuanza sehemu ya pili ya Kazi Yangu juu ya wanadamu, kuwaruhusu watu wote wanifuate kwa karibu ili washirikiane na Kazi Yangu, na kuwaruhusu watu kufanya yote katika uwezo wao kufanya Nami kazi Ninayopaswa kufanya.

Hakuna aliye na imani kwamba atauona utukufu Wangu, na Mimi Siwalazimishi. Mimi Nauondoa utukufu Wangu kutoka miongoni mwa watu hao na kuchukua kwa ulimwengu mwingine. Wakati watu wanatubu tena, basi Mimi Nitaonyesha utukufu Wangu kwa zaidi ya wale wanaoamini. Hii ni kanuni ambayo Mimi hufuata katika kazi Yangu. Kwa maana kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaondoka Kanaani, na pia kuna wakati ambapo utukufu Wangu unawaacha waliochaguliwa. Aidha, kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaiacha dunia nzima, kiasi kwamba itakuwa hafifu na kutumbukia katika giza. Hata nchi ya Kanaani haitaona mwanga wa jua; watu wote watapoteza imani yao, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kuiacha harufu nzuri ya nchi ya Kanaani. Nitakapopita katika mbingu mpya na nchi tu ndipo Nitakapofichua sehemu nyingine ya utukufu Wangu kwanza katika nchi ya Kanaani, kuruhusu mwanga kuangazia dunia nzima ikiwa giza kama usiku, ili kwamba dunia nzima iujie mwanga huo. Wacha watu wote duniani kote waje kuteka nguvu za mwanga, kuruhusu utukufu Wangu uongezeke na kuonekana upya kwa mataifa yote. Wacha watu wote watambue kwamba muda mrefu uliopita Nilikuja duniani na muda mrefu uliopita Nilileta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki; kwa maana utukufu Wangu unang'aa kutoka Mashariki, ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo. Lakini Nilitokea Israeli na kutoka huko Nikawasili Mashariki. Wakati mwanga wa Mashariki unapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani linaanza kugeuka na kuwa mwanga, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba nilishatoka Israeli na Nimeanza kuchomoza upya katika Mashariki. Niliwahi shuka katika Israel na baadaye Niliondoka. Kwa sababu hii, [b] Siwezi tena kuzaliwa huko kwa mara nyingine, kwa ajili kazi Yangu inaongoza ulimwengu mzima na umeme unaangaza kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Mimi Nimeshuka katika Mashariki na kuwaletea Kanaani watu wa Mashariki. Ningependa kuleta watu kutoka dunia nzima katika nchi ya Kanaani, hivyo Mimi Naendelea kutoa sauti Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna mwanga katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli Mashariki, na kuwaleta watu wote Mashariki. Nimewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta kuuona mwanga tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha kuona kwamba tayari Nimeshuka chini juu ya wingu jeupe miongoni mwa watu, na kuona mawingu mengi meupe na vishada vya matunda, na zaidi ya hayo, Yehova, Mungu wa Israeli. Nami Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi Aliyengojewa, na kuonekana kamili kwa mimi Niliyeteswa na wafalme katika enzi zote. Nitafanya kazi ya ulimwengu mzima na kufanya kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambaye amengoja Nionekane kwa mara nyingine tena, na kwa watu wote walionitesa Mimi, ili wote wajue kwamba Mimi kwa muda mrefu uliopita Nimeuchukua utukufu Wangu na kuuleta katika Mashariki. Hauko katika Yudea, kwa maana siku za mwisho tayari zimewadia!

Katika ulimwengu mzima Mimi Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, kutikisa dini zote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo iliyoleta watu katika wakati wa sasa. Nimeiwacha sauti Yangu kuwa inayowashinda wanadamu; wote wanaingia katika mkondo huu na wote wananyenyekea mbele Zangu, kwa maana Mimi kwa muda mrefu uliopita Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote na Nikaupeleka upya Mashariki. Ni nani asiye na hamu ya kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuuona uzuri Wangu? Ni nani asiyetaka kuja kwenye mwanga? Ni nani asiyeona utajiri wa Kanaani? Ni nani asiyengoja kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mkuu Mwenyezi? Sauti Yangu lazima ienee kote duniani; Ningependa kuzungumza zaidi na watu Wangu wateule. Maneno Ninayotamka yanatikisa milima na mito kama radi yenye nguvu; Nasema na ulimwengu wote na kwa watu wote. Hivyo maneno Yangu yanakuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni jinsi kwamba mtu huchukia kuyaacha na pia kuyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote, mwanadamu anayafurahia. Kama watoto wachanga waliozaliwa karibuni, watu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sababu ya sauti Yangu, Nitawaleta watu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia kirasmi kati ya wanadamu ili waje kuniabudu Mimi. Utukufu Ninaotoa na maneno Yangu yatawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki, na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye "Mlima wa Mizeituni" wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari kwa muda mrefu Nimekuwa duniani, si tena Mwana wa Wayahudi lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwa maana ni muda mrefu tangu Nimekwishafufuka, Nimekwenda kutoka miongoni mwa wanadamu, na Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu kwa utukufu. Mimi ndiye Nilichiwa kabla ya enzi, na "mtoto mchanga" aliyeachwa na Israeli kabla ya enzi. Aidha, Mimi ndimi mwenye utukufu wote mtukufu Mwenyezi Mungu wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, kusikia sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vile vile madhumuni ya usimamizi Wangu. Basi kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na kila mtu awe mmoja wa wale walio chini Yangu!

Maelezo ya Chini:

a. Nakala ya awali haina "kuona kwamba."

b. Nakala ya awali haina "Kwa sababu hii."