Sura ya 16

Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao. Nitakapoondoka duniani ndipo haswa Nitakapopanda kwa kiti cha enzi katika moyo wa binadamu, yaani, itakuwa wakati watu wote watanijua Mimi. Hivyo pia, itakuwa wakati wana Wangu na watu watatawala dunia. Wale ambao wananijua Mimi bila shaka watakuwa nguzo za ufalme Wangu, na wao peke yao ndio watastahiki kutawala na kuwa na mamlaka katika ufalme Wangu. Wote ambao wananijua Mimi wana nafsi Yangu, na wana uwezo wa kuishi kwa kunidhihirisha miongoni mwa watu wote. Sijali mwanadamu ananijua Mimi kwa kiwango gani: Hakuna yeyote anayeweza kuzuia kazi Yangu kwa njia yoyote, na mwanadamu hawezi kunipa usaidizi wowote wala kunifanyia lolote. Mwanadamu anaweza tu kufuata mwongozo Wangu katika mwangaza Wangu, na kutafuta matakwa Yangu kwenye mwangaza huu. Leo, watu wana sifa zinazostahili, na wanaamini wanaweza kutembea kwa maringo mbele Yangu, na kucheka na kufanya mzaha na Mimi bila kizuizi hata kidogo, na kunihutubia Mimi kama tuko sawa. Bado mwanadamu hanijui Mimi, bado anaamini kuwa kiasili sisi kadri tuko sawa, kuwa sisi sote ni nyama na damu, na sote tunaishi katika dunia ya binadamu. Uchaji wake Kwangu ni mdogo sana; ananiheshimu Mimi anapokuwa mbele Yangu, lakini hawezi kunihudumia Mimi mbele ya Roho. Ni kama, kwa mwanadamu, Roho hayupo kabisa. Kwa hivyo, hakuna mwanadamu ashawahi kumjua Roho; katika kupata mwili Kwangu, watu huona tu mwili wa nyama na damu, na hawamtambui Roho wa Mungu. Matakwa Yangu yanaweza kutimizwa kwa njia kama hii? Watu ni mabingwa wa kunihadaa Mimi; wanaonekana kama ambao wamepewa mafunzo maalum na Shetani ili kunihadaa Mimi. Lakini Shetani bado hanibabaishi Mimi. Bado Nitatumia hekima Yangu kuwashinda wanadamu wote na kumshinda ambaye anawapotosha wanadamu wote, ili ufalme Wangu uanzishwe duniani.

Miongoni mwa binadamu, kuna wale ambao wamejaribu kujua ukubwa wa nyota, au upana wa mbingu. Lakini utafiti wao haujawahi kuweza kuzaa matunda, na hawana hiari ila tu kuinamisha vichwa vyao kwa masikitiko na kukubali kushindwa. Nikiwaangalia watu wote na kuchunguza uwezo wa mwanadamu katika kushindwa kwake, Sioni yeyote yule ambaye ameniamini kabisa, hakuna ambaye ananitii Mimi na kujinyenyekeza Kwangu. Matarajio ya wanadamu ni yasiyo ya kawaida kweli! Wakati yote yalikuwa yamefunikwa na kiza, miongoni mwa wanadamu Nilianza kuonja uchungu wa dunia. Roho Wangu husafiri kote duniani na kuangalia ndani ya nyoyo za watu wote, na bado pia, Mimi huwashinda wanadamu katika mwili wangu wa nyama. Mwanadamu huwa hanioni Mimi, kwa kuwa yeye ni kipofu; mwanadamu hanijui Mimi, kwani amekuwa hana hisia; mwanadamu hunipinga Mimi, kwa kuwa yeye si mtiifu; mwanadamu huja kusujudu mbele Yangu, kwa kuwa ameshindwa na Mimi; mwanadamu huja kunipenda Mimi, kwa kuwa Nastahili kiasili kupata upendo wa mwanadamu; mwanadamu huishi kulingana na Mimi na kunidhihirisha Mimi, kwa sababu nguvu Zangu na hekima Yangu humfanya apendeze nafsi Yangu. Nina nafasi katika moyo wa mwanadamu, lakini kamwe Sijawahi kupokea upendo wa mwanadamu Kwangu katika roho yake. Kwa kweli, kuna mambo katika roho ya mwanadamu anayoyapenda kuliko yote mengine, lakini Mimi si mojawapo wa mambo hayo, na kwa hivyo upendo wa mwanadamu ni kama kiputo cha sabuni: Upepo unapovuma, hukipasua na kinaenda, kisiwahi kuonekana tena. Mtazamo Wangu kuhusu mwanadamu siku zote umekuwa thabiti na usiobadilika. Kuna yeyote kati ya wanadamu, ambaye angeweza kufanya vivyo hivyo? Machoni pa mwanadamu, Mimi sigusiki wala Mimi sionekani mithili ya hewa, na kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu hutafuta tu katika anga isiyokuwa na mipaka, au juu ya bahari ambayo si tulivu, au juu ya ziwa tulivu, au miongoni mwa maandiko na mafundisho matupu. Hakuna mtu hata mmoja anayejua kiini cha binadamu, sembuse yeyote anayeweza kusema chochote kuhusu fumbo lililo ndani Yangu, na kwa hivyo huwa Simtaki mwanadamu afikie viwango vya juu zaidi ambavyo yeye hudhani Nahitaji kutoka kwake.

Ndani ya maneno Yangu, milima hupinduliwa, maji hutiririka kinyumenyume, mwanadamu huwa mtiifu, na maziwa huanza kutiririka bila kusita. Ingawa bahari isiyo tulivu huenda kwa hasira kuelekea mbinguni, ndani ya maneno Yangu bahari za aina hii hutulia kama upande wa juu wa ziwa. Kwa kupunga mkono Wangu kidogo tu, upepo mkali kabisa hutokomea na kutoka Kwangu mara moja, na ulimwengu wa mwanadamu hurejesha utulivu wake mara moja. Lakini Ninapotoa ghadhabu Yangu, milima hutenganishwa mara moja, ardhi huanza kutetemeka mara moja, maji hukauka mara moja, na mwanadamu huzingirwa na maafa mara moja. Kwa ajili ya ghadhabu Yangu, huwa Mimi sisikilizi vilio vya mwanadamu, huwa sitoi msaada ili kujibu vilio vyake, kwani hasira Yangu inapanda. Ninapokuwa miongoni mwa mbingu, nyota hazijawahi kutishiwa na kuwepo Kwangu kamwe. Bali, huwa zinaweka nyoyo zao katika kunifanyia kazi Mimi, na kwa hivyo, Mimi huzipa mwangaza zaidi na kuzifanya zing’are zaidi, ili zipate utukufu zaidi kwa ajili Yangu. Kadri mbingu inavyong’aa zaidi, ndivyo dunia chini yake inazidi kuwa na giza; watu wengi sana hulalamika kuwa mipango Yangu huwa haifai, wengi wameniacha kuunda ufalme wao wenyewe, ambao wanautumia kunisaliti, na kubadili hali ya giza. Ila nani ameweza kutimiza hili kwa azma yao? Ni nani ametimiza hili kwa azimio lake? Nani anaweza kubadili yale ambayo yamepangwa na mkono Wangu? Wakati majira ya machipuko yanaenea kwenye ardhi, Mimi hupeleka mwangaza kwa siri na kimya ulimwenguni, ili, duniani, mwanadamu awe na hisia ya ghafla ya usafi hewani. Hata hivyo, wakati huo huwa Ninafunika macho ya mwanadamu, ili aone tu ukungu ukiwa umefunika ardhi, na watu na vitu vyote havibainiki. Watu kupumua tu kwa masikitiko. Mbona mwangaza uling’aa kwa muda mdogo tu? Kwa nini Mungu humpa binadamu ukungu na utusitusi tu? Huku watu wakikata tamaa, ukungu hupotea mara moja, lakini wanapoona dalili ya mwangaza, Mimi huachilia mbubujiko wa mvua juu yao, na viwambo vyao vya masikio vinavunjwa kwa ajili ya mvua na radi wanapolala. Huku wakiwa na hofu, hawana wakati wa kujikinga, na hugubikwa na mvua kubwa. Papo hapo, yote yaliyo chini ya mbingu hufagiliwa katika ghadhabu Yangu yenye hasira. Watu hawalalamiki tena kuhusu mwanzo wa mvua kubwa, na ndani yao wote, uchaji huzaliwa. Kwa sababu ya uvamizi huu wa ghafla wa mvua, idadi kubwa ya watu wanazama ndani ya maji yanayonyesha kutoka mbinguni, na kuwa maiti ndani ya maji. Naangalia dunia nzima na kuona kuwa wengi wanazinduka, kuwa wengi wanatubu, kuwa wengi wanatafuta chanzo cha maji ndani ya mashua ndogo, kuwa wengi wananisujudu Mimi ili kuomba msamaha Wangu, kuwa wengi wameona mwangaza, kuwa wengi wameona uso Wangu, kuwa wengi wana ujasiri wa kuishi, na kuwa ulimwengu mzima umebadilishwa. Kufuatia mbubujiko huu mkubwa wa mvua, vitu vyote vimerudi kuwa jinsi vilivyokuwa katika akili Yangu, na haviasi tena. Kabla ya muda mrefu, ardhi yote imejaa sauti za vicheko, na kila mahali duniani kuna hali ya sifa, na hakuna popote ambapo hapana utukufu Wangu. Hekima Yangu iko kote duniani, na katika ulimwengu mzima. Miongoni mwa vitu vyote, kuna matunda ya hekima Yangu, miongoni mwa watu wote, kumejaa kazi bora zaidi za hekima Yangu; kila kitu ni kama mambo yote katika ufalme Wangu, na watu wote wanakaa kwa mapumziko chini ya mbingu Zangu kama kondoo kwenye uwanja Wangu wa malisho. Nasonga juu ya wanadamu wote na Natazama kila mahali. Hakuna kinachokaa kizee kamwe, na hakuna mtu ambaye yuko kama alivyokuwa. Ninapumzika katika kiti cha enzi, Naegemea juu ya ulimwengu mzima, na Nimeridhika kikamilifu, kwani kila kitu kimerejesha utakatifu wake, na Ninaweza kukaa kwa amani ndani ya Zayuni tena, na watu duniani wanaweza kuishi maisha tulivu na ya kuridhisha chini ya mwongozo Wangu. Watu wote wanasimamia kila kitu mikononi Mwangu, watu wote wamerejesha akili zao za awali na mwonekano wao wa kiasili; hawafunikwi tena na vumbi, lakini, ndani ya ufalme Wangu, ni safi kama lulu, kila mmoja akiwa na uso kama vile wa yule mtakatifu aliye ndani ya moyo wa binadamu, kwani ufalme Wangu umeimarishwa miongoni mwa binadamu.

Machi 14, 1992

Iliyotangulia: Sura ya 15

Inayofuata: Sura ya 17

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp