Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote, mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli mkamilifu! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vitasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi. Ee, Mwenyezi Mungu! Wewe ni kila kitu, Wewe umetimiza kila kitu, na kila kitu kinakamilika na Wewe, vyote vinang’aa, vyote vimekombolewa, vyote viko huru, vyote viko imara na vyenye nguvu! Hakuna chochote kilichofichwa wala kufungwa, na Wewe mafumbo yote yanafumbuliwa. Zaidi ya hayo, Wewe unahukumu halaiki ya adui Zako, unaonyesha Ukuu wako, unaonyesha moto Wako wenye ghadhabu, unaonyesha ghadhabu Yako, na hata zaidi Unaonyesha utukufu Wako isiyo ya kifani, idumuyo na isio na mwisho! Watu wote wanapaswa kuamka na wanapaswa kushangilia na kuimba bila kusita, wakihimidi mwenye Uweza, yule wa kweli, anayeishi, mkarimu, adhimu na Mungu wa kweli aliye kutoka milele hadi milele. Kiti Chake cha enzi kinapasa kutukuzwa kila wakati, jina Lake takatifu kusifiwa na kutukuzwa. Haya ni mapenzi ya milele ya—Mungu Wangu na ni baraka zisizo na mwisho ambazo Yeye hufichua na kutukarimia! Je, ni nani kati yetu ambaye hairithi? Ili kurithi baraka za Mungu, mtu lazima alitukuze jina takatifu la Mungu na kuja kumwabudu kwa kuzunguka kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wanaenda mbele Yake wakiwa na nia nyingine na dhamira nyingine wanayeyushwa na moto Wake wenye ghadhabu. Leo ni siku ambayo adui Zake watahukumiwa, na pia wataangamia katika siku hii. Hata zaidi ni siku ambayo Mimi, Mwenyezi Mungu, atafunuliwa na siku ambayo Atapokea utukufu na heshima. Ee, watu wote! Inukeni haraka ili mhimidi na kumkaribisha Mwenyezi Mungu ambaye milele na milele hutupa wema wenye upendo, wokovu, na kutupa baraka, huwafanya wana Wake kuwa wakamilifu na kufikia ufalme Wake kwa mafanikio! Hili ni tendo la ajabu la Mungu! Haya ni majaaliwa ya milele wa Mungu na mpango, kwamba Yeye Mwenyewe aje kutuokoa, kutufanya wakamilifu na kutuleta kwenye utukufu.

Wale wote ambao hawainuki na kuwa na ushuhuda ni wahenga wa vipofu, wafalme wa wasiojua na watakuwa daima wasiojua, wajinga wa milele na vipofu waliokufa daima. Kwa hivyo nafsi zetu zinapasa kuamka! Watu wote wanapaswa kuinuka! Shangilia, sifu na kuhimidi bila kikomo Mfalme wa utukufu, Baba wa huruma, Mwana wa ukombozi, Roho saba zenye ukarimu, na Mwenyezi Mungu anayeleta moto adhimu wenye ghadhabu na hukumu yenye haki, anayejitosheleza, mkarimu, mwenye Uweza, na mkamilifu. Kiti Chake cha enzi kitatukuzwa milele! Watu wote wanafaa kuona kwamba hii ni hekima ya Mungu, ni njia Yake ya shani ya wokovu, na utimilifu wa mapenzi Yake yenye utukufu. Tusipoinuka na kuwa na ushuhuda, wakati muda utakapokwisha basi hakutakuwa na kurudi nyuma. Iwapo tunapokea baraka au balaa inaamuliwa katika hatua hii iliopo ya safari yetu, kulingana na tunayotenda, fikiria au kuishi wakati huu. Basi mnapaswa kutenda yapi? Kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kumtukuza Mungu milele, kutukuza mwenye Uweza Kristo—Mungu wa kweli, wa kipekee, na wa milele!

Kuanzia sasa kuendelea unapaswa kuona wazi kuwa wale wote wasiokuwa na ushuhuda kwa Mungu, wasiokuwa na ushuhuda kwa wale wa kipekee, waaminifu kwa Mungu, wale wanaohifadhi tashwishi kuhusu Yeye, wote ni wagonjwa, wafu na wenye kumuasi Mungu! Maneno ya Mungu yamehakikishwa kutoka nyakati za kale: Wale wote ambao hawakusanyi na Mimi wanatawanyika, na wale wasio upande Wangu wako dhidi Yangu; huu ni ukweli usioweza kubadilishwa uliochongwa jiweni! Wale wasiokuwa na ushuhuda kwa Mungu ni vikaragosi wa Shetani. Watu hawa huja kuwasumbua na kuwadanganya watoto wa Mungu, kukatiza usimamizi wa Mungu, na sharti wawekwe kwenye upanga! Yeyote anayewaonyesha nia nzuri anatafuta maangamizi yake mwenyewe. Unapaswa kusikiza na kuamini tamko la Roho wa Mungu, kutembea kwenye njia ya Roho wa Mungu na kuishi kwa maneno ya Roho wa Mungu, na hata zaidi kusifu kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu milele!

Mwenyezi Mungu ni Mungu wa Roho saba! Yeye pia ni Mungu wa[a] macho saba na nyota saba, Yeye hufungua muhuri saba, na hati ya kukunja inafunguliwa na Yeye! Amepiga baragumu saba, na vitasa saba na mapigo saba yako mikononi Mwake, yatakayofunguliwa kwa mapenzi Yake. Ee, ngurumo saba ambazo daima zimefungwa! Wakati wa kuzifungua umewadia! Yule atakayezifungua ngurumo saba tayari ameshaonekana mbele ya macho yetu!

Mwenyezi Mungu! Kila kitu kimekombolewa na kuwa huru na Wewe, hapana ugumu, na kila kitu kinakwenda vizuri! Hakuna kinachothubutu kukupinga au kukuzuia Wewe, vyote hukutii. Chochote kisichotii hufa!

Mwenyezi Mungu, Mungu mwenye macho saba! Vyote viko wazi vikamilifu, vyote ni ng’avu na wazi, vyote vimefunuliwa na kuwekwa wazi. Vyote ni dhahiri kabisa na Yeye, na si tu kuwa Mungu Mwenyewe yuko hivi, lakini pia wana Wake wako hivi vilevile. Hapana yeyote, hakuna kitu chochote, na hakuna hoja yoyote inayoweza kufichwa mbele Yake na wana Wake!

Nyota saba za Mwenyezi Mungu ni ng’avu bashashi! Kanisa limefanywa kuwa kamili na Yeye, Yeye huweka imara mitume wa kanisa Lake na kanisa lote liko ndani ya utoaji Wake. Yeye anafungua mihuri yote saba, na Yeye Mwenyewe analeta mpango wa usimamizi Wake na mapenzi Yake hadi tamati. Hati ndiyo kunga ya lugha ya kiroho ya usimamizi Wake na Amekifungua na kukifunua!

Watu wote wanapaswa kusikia baragumu Zake saba zinazopigwa kwa sauti. Kwake vyote ninawekwa vinajulishwa, kamwe kutofichwa ama kuwa na huzuni tena. Vyote vinafunuliwa na vyote vinashinda!

Baragumu saba za Mwenyezi Mungu ziko wazi, baragumu adhimu na zenye ushindi! Pia ni baragumu zinazowahukumu adui Zake! Katikati ya ushindi Wake, baragumu Yake inatukuzwa! Yeye hutawala ulimwengu mzima!

Yeye amevitayarisha vitasa saba vya mapigo na vyote vinafunguliwa kwa nguvu kabisa kwa adui Zake kwa kiwango cha juu, na watateketea kwa miale ya moto Wake wenye ghadhabu. Mwenyezi Mungu huonyesha uwezo wa mamlaka Yake na adui Zake wote wanaangamia. Ngurumo saba za mwisho hazitafichwa tena mbele ya Mwenyezi Mungu, zote ziko wazi! Zote ziko wazi! Yeye huwaua adui Zake kwa ngurumo saba, Akiimarisha dunia, Akiifanya itoe huduma Kwake, kamwe kutokuwa isiyofaa!

Mwenyezi Mungu mwenye haki! Tunakutukuza milele! Unastahili sifa zisizoisha, kuhimidiwa kusikoisha na kutukuzwa! Ngurumo Zako saba si tu za hukumu Yako, bali zaidi ni kwa ajili ya utukufu na mamlaka Yako, ili kukamilisha vitu vyote!

Watu wote wanasherehekea mbele ya kiti cha enzi, wakikuhimidi na kukutukuza kwa shangwe Kristo Mungu mwenye uweza! Sauti zao zinarindima kama radi! Bila shaka vitu vyote vinakuwepo kwa ajili Yake, na kuinuka kwa ajili Yake. Je, ni nani anayethubutu kutoona utukufu, heshima, mamlaka, hekima, utakatifu, ushindi na ufunuo kuwa sio Zake? Hii ndiyo utimilifu wa mapenzi Yake na kukamilika kwa mwisho kwa uundaji wa usimamizi Wake!

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “Mungu wa.”

Iliyotangulia:Sura ya 33

Inayofuata:Sura ya 35

Maudhui Yanayohusiana