755 Ni Wale tu Wanaomshinda Shetani Ndio Wanaookolewa

1 Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia.

2 Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari.

3 Kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 754 Mungu Atawapata tu Wale Wanaomshinda Shetani Kabisa

Inayofuata: 756 Mshinde Shetani kwa Ukweli ili Upatwe na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp