376 Wale Wasiomtii Mungu Wanamsaliti
1 Tabia ambayo haiwezi kunitii kabisa ni usaliti. Mwenendo ambao hauwezi kuwa mwaminifu Kwangu ni usaliti. Kunidanganya na kutumia uongo kunilaghai ni usaliti. Kujawa na dhana na kuzieneza kila mahali ni usaliti. Kutozilinda shuhuda na maslahi Yangu ni usaliti. Kubuni tabasamu wakati mtu ameniacha moyoni mwake ni usaliti. Tabia hizi ni mambo yote ambayo daima mna uwezo wa kuyafanya, na pia ni za kawaida kati yenu. Hakuna mmoja wenu anayeweza kufikiri kwamba hilo ni tatizo, lakini Mimi sifikirii hivyo. Siwezi kuchukulia kunisaliti kama jambo dogo, na zaidi ya hayo siwezi kulipuuza. Sasa, Nafanyapo kazi miongoni mwenu, mnakuwa wenye tabia ya aina hii—ijapo siku ile ambapo hakutakuwa na mtu wa kuwalinda, hamtakuwa kama wezi waliojitangaza kuwa wafalme? Wakati hili linafanyika na mnasababisha janga kubwa, nani atakuwa hapa kuvisafisha vitu tena na kuondoa uchafu?
2 Mnaweza kufikiri kwamba baadhi ya vitendo vya usaliti ni kitu cha mara moja tu badala ya tabia ya kuendelea, na hakipaswi kutajwa kwa uzito hivi, kikiwasababisha kuadhirika. Kama kweli mnaamini hivyo, basi mnakosa wepesi wa kuhisi. Kadiri mtu anavyofikiri hivi, ndivyo anavyokuwa kielelezo na umboasili wa uasi. Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana.
Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili