369 Walio Gizani Wanapaswa Kuinuka
1 Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi, wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida. Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu?
2 Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake.
Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili