805 Ni Wale tu Wanaomjua Mungu Ndio Wanaweza Kumshuhudia

1 Sababu ya wale ambao humshuhudia Mungu wanaweza kumtolea ushuhuda wa kufana ni kwa kuwa ushuhuda wao umekitwa kwenye msingi wa ufahamu wa kweli pamoja na matamanio ya kweli kwa Mungu, si kutokana na msukumo wa hisia, lakini kulingana na ufahamu wa Mungu na tabia Zake. Kwa sababu wamepata kumjua Mungu, wanahisi kwamba lazima wamshuhudie Mungu, na kuwafanya wale wote wamtamanio Mungu wamjue Mungu, na kufahamu upendo wa Mungu, na uhalisi Wake.

2 Sawa na mapenzi ya watu kwa Mungu, ushuhuda wao ni wa hiari, ni halisi, na una umuhimu halisi na thamani. Si baridi, au tupu na usiokuwa na maana. Sababu ya wale tu wanaompenda Mungu kweli kuwa na thamani na maana katika maisha yao, na kuamini katika Mungu tu, ni kwa sababu watu hawa wanaishi katika mwangaza wa Mungu, na wanaweza kuishi kwa ajili ya kazi ya Mungu na usimamizi Wake; hawaishi gizani, bali wanaishi katika mwangaza; hawaishi maisha yasiokuwa na maana, ila wanaishi maisha ambayo yamebarikiwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 804 Matokeo Yanayofanikishwa na Kumjua Mungu

Inayofuata: 806 Matokeo ya Kutojua Tabia ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp