343 Wasiomjua Mungu Humpinga Mungu

1 Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu.

2 Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

3 Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa kishindo na tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 342 Mungu Huchukia Hisia Kati ya Watu

Inayofuata: 344 Yeyote Anayempima Mungu Kwa Fikira Anampinga Yeye

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp