845 Ni Wale tu Wanaokamilishwa na Mungu Wanaweza Kumpenda kwa Kweli

1 Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani. La sivyo, upendo wake si safi, ni upendo wa kishetani, na ule ambao hauwezi kabisa kupokea idhini ya Mungu.

2 Kama binadamu hakamilishwi, kushughulikiwa, kuvunjwa, kupogolewa, kufundishwa nidhamu, kuadibiwa, au kusafishwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja, hakuna yeyote anayeweza kumpenda Mungu kwa kweli. Ukisema kwamba sehemu ya tabia yako inamwakilisha Mungu na hivyo basi unaweza kumpenda Mungu kwa kweli, basi wewe ndiwe unayezungumza maneno ya kiburi na ni binadamu wa upuuzi. Binadamu kama hao ni malaika mkuu! Asili ya ndani ya binadamu haiwezi kumwakilisha Mungu kwa njia ya moja kwa moja. Lazima binadamu aiondoe asili yake ya ndani kupitia kwa ukamilifu wa Mungu, na kisha kupitia kutunza na kutosheleza mapenzi ya Mungu tu, na hata zaidi kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu, ndipo kuishi kwa kudhihirishwa kwake kunaweza kuidhinishwa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 844 Mungu Atakukamilisha Ukiitembea Tu Njia ya Petro

Inayofuata: 846 Watu Waliokamilishwa na Maneno ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp