742 Ni Wale tu Wanaomcha Mungu Ndio Wenye Furaha

1 Ayubu alikuwa mwanamume aliyemcha Mungu na aliyeambaa maovu alipokuwa hai; Mungu alimpongeza kwa matendo yake ya haki, watu waliyakumbuka, na maisha yake, zaidi ya yeyote yule mwingine, yalikuwa na thamani na umuhimu. Ayubu alifurahia baraka za Mungu na aliitwa mtakatifu na Yeye hapa duniani, na aliweza pia kujaribiwa na Mungu na kujaribiwa na Shetani; alisimama kuwa shahidi wa Mungu na alistahili kuwa mtu mtakatifu. Kwenye miongo mbalimbali baada ya kujaribiwa na Mungu, aliishi maisha ambayo yalikuwa yenye thamani zaidi, yenye maana zaidi, yaliyokita mizizi, na yenye amani zaidi kuliko hata awali. Ayubu aliishi maisha kwenye harakati ya kutafuta kimsingi kusadiki, utambuzi, na unyenyekevu kwa ukuu wa Mungu, na ilikuwa katika kusadiki huku, utambuzi huu na unyenyekevu huu ambapo aliweza kupitia zile awamu muhimu za maisha, aliishi kwa kudhihirisha miaka yake ya mwisho na akajuliana hali na awamu yake ya mwisho ya maisha.

2 Licha ya kile ambacho Ayubu alipitia, bidii zake na shabaha zake katika maisha zilikuwa za furaha na wala si zenye maumivu. Alikuwa na furaha si tu kwa sababu ya baraka au shukrani aliyopewa yeye na Muumba, lakini muhimu zaidi kwa sababu ya shughuli zake na shabaha za maisha, kwa sababu ya maarifa yaliyoongezeka kwa utaratibu na ufahamu wa kweli wa ukuu wa Muumba ambao alitimiza kupitia kwa kumcha Mungu na kwa kuepuka maovu, na zaidi, kwa sababu ya matendo Yake ya maajabu ambayo Ayubu alipitia kibinafsi wakati huu akiwa chini ya ukuu wa Muumba, na hali aliyopitia yenye uchangamfu na isiyosahaulika na kumbukumbu za kuwepo kwake, kuzoeana na wenzake, na kuzoeana kati yake yeye na Mungu; kwa sababu ya tulizo na furaha zilizotokana na kujua mapenzi ya Muumba; kwa sababu ya kustahi kulikotokea baada ya kuona kwamba Yeye ni mkubwa, ni wa ajabu, Anayependeka, na ni mwaminifu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 741 Mche Mungu Upate Ulinzi Wake

Inayofuata: 743 Ni Wale Tu Wamchao Mungu Ambao Huishi Kwa Heshima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp