992 Maonyo Matatu ya Mungu kwa Mwanadamu
Ni muhimu sana kwamba Mungu alikuja kwa wanadamu kwa njia ya kuwa mwili na kazi aliyofanya katika mwili ni muhimu sana pia. Na, tabia Aliyoifichua na mapenzi Alionyesha ni muhimu hata sana kwa kila mtu anayeishi katika mwili, kwa kila mtu anayeishi katika upotovu. Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa? Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, umefanya hitimisho lolote kuhusiana na namna unavyofaa kumtunza Mungu? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili utende, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anafanya na wewe, kile Anachopanga na wewe, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi.
Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili