1000 Wakati wa Kuachana

1 Katika wakati wa uumbaji, Nilikuwa nimetabiri kwamba katika siku za mwisho Nitafanya kundi la watu ambao wana nia moja na Mimi. Nilikuwa nimetabiri kwamba baada ya kuanzisha mfano duniani katika siku za mwisho, Nitarudi kwenye makao Yangu. Wakati wanadamu wote wameniridhisha Mimi, watakuwa wametimiza matakwa Yangu, na Mimi Sitahitaji tena kitu chochote kutoka kwao. Badala yake, wanadamu na Mimi tutasimuliana hadithi za siku zetu za zamani na baada ya hapo tutaagana. Natumaini kwamba baada ya sisi kutengana, wanadamu wanaweza kutekeleza “urithi” Wangu na kutosahau kuhusu mafundisho ambayo Nimetoa wakati wa maisha Yangu, kutofanya lolote ambalo lingeleta aibu kwa jina Langu, na kukumbuka neno Langu. Natumaini kwamba binadamu watajitahidi kabisa kuniridhisha Mimi Nitakapokuwa Nimeondoka. Natumaini kuwa binadamu watatumia neno Langu kama msingi wa maisha yao. Msinivunje moyo kwa sababu moyo Wangu daima umekuwa ukiwajali wanadamu na Mimi Nimewapenda daima.

2 Binadamu na Mimi tulikusanyika pamoja wakati mmoja na kufurahia duniani baraka hizo hizo zilizo mbinguni. Niliishi pamoja na wanadamu na kukaa pamoja nao, wanadamu walinipenda daima, nami Niliwapenda daima; tulikuwa na uhusiano kati yetu. Ninapokumbuka wakati Wangu pamoja na wanadamu, Nakumbuka siku zetu zikijawa na kicheko na furaha, na zaidi ya hayo, kulikuwa na ugomvi. Hata hivyo, upendo kati yetu uliimarishwa kwa msingi huu na kushughulikiana kwetu hakukuwahi kuvunjika. Kati ya miaka yetu mingi ya mawasiliano, wanadamu wameacha alama kubwa juu Yangu nami Nimewapa wanadamu mambo mengi ili wafurahie, ambayo wanadamu daima wameonyesha shukrani kubwa kuyahusu. Sasa, mkutano wetu ni tofauti na kitu chochote cha awali; nani angeweza kukosa wakati huu wa kuagana kwetu? Wanadamu wananipenda sana, nami Nina upendo usio na mwisho kwao, lakini ni nini kinaweza kufanywa kuhusu hilo? Nani angethubutu kwenda kinyume na mahitaji ya Baba wa mbinguni?

3 Nitarejea kwenye makao Yangu, ambapo Nitakamilisha sehemu nyingine ya kazi Yangu. Pengine tutapata nafasi ya kukutana tena. Ni matumaini yangu kuwa wanadamu hawatahisi huzuni sana na kwamba wataniridhisha Mimi duniani; mara nyingi Roho Wangu aliye mbinguni Atawapa neema. Yaache mambo yote mabaya yaliyotokea kati yetu yawe katika wakati uliopita, acha kuwe na upendo kati yetu daima. Nimewapa wanadamu upendo mwingi sana na wanadamu wamelipa gharama kubwa sana kwa ajili ya kunipenda Mimi. Hivyo, Natumaini kwamba binadamu watathamini upendo safi na takatifu kati yetu ili upendo wetu uenee kote katika dunia ya wanadamu na kupitishwa kwa vizazi vingine milele. Tutakapokutana tena, hebu tuungane katika upendo ili upendo wetu uweze kuendelea milele na kusifiwa na kuzungumziwa na watu wote. Hili lingeniridhisha na Ningewaonyesha wanadamu uso Wangu wenye tabasamu. Natumaini kwamba wanadamu watakumbuka yote Niliyowakabidhi.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 47” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 999 Wote Wasiotenda Ukweli Lazima Wakutane na Maangamizo

Inayofuata: 1001 Matamshi ya Mungu ni Ushawishi Bora kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp