120 Kumpenda Mungu ni Tamanio la Moyo Wangu

1

Kuishi katika ulimwengu huu mpana, sikuwahi tambua ukweli.

Baada ya kusoma neno la Mwenyezi Mungu tu ndipo nilijua maana ya maisha.

Nuru ya kweli imekuja ulimwenguni, na Kristo ni ukweli, njia, na uzima.

Nikifurahia kunyunyiziwa maji na chakula cha neno la Mungu, nilipata njia ya uzima wa milele.

Nikitenda na kupitia maneno ya Mungu, nimekua polepole katika maisha.

Ninathamini ukweli, ninathamini neno la Mungu.

Kristo ni Mungu wa vitendo, ninatoa sifa na shukurani zangu.

Kumpenda Mungu ni tamanio langu, shauku la moyo wangu. Aleluya!

2

Neno la Mungu linafichua ukweli na chanzo cha upotovu wa mwanadamu.

Mwanadamu ni fidhuli, mwenye ubinafsi na mdanganyifu, hana dhamiri wala mantiki.

Nikikabiliana na hukumu mbele ya kiti cha Kristo, nimeonja haki na tabia adhimu ya Mungu.

Nimepata uchaji na upendo kwa Mungu, na ninanyenyekea mbele Yake kweli.

Nilitoka mavumbini, maskini na mwenye kusikitisha, bila chochote.

Neno la Mungu limenitakasa, sasa ninaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu.

Kristo ni Mungu wa vitendo, anayestahili upendo wa mwanadamu.

Kumpenda Mungu ni tamanio langu, shauku la moyo wangu. Aleluya!

3

Kristo kuonyesha ukweli wote hunifanya nione mwanga maishani.

Ninapata hukumu na utakaso wa maneno ya Mungu, tabia yangu imebadilika.

Mungu huninitolea ukweli kama maisha, ili niweze kupatana na Yeye.

Kila neno la Mungu ni ukweli, ulio moyoni mwangu.

Nikitenda na kupitia maneno ya Mungu, hatimaye najua ukweli ni uzima na wa thamani sana.

Neno Lake ndilo lililonibadilisha, likanipa maisha mapya.

Kristo ni Mungu wa vitendo, tamanio langu ni kumpenda milele.

Kumpenda Mungu ni tamanio langu, shauku la moyo wangu. Aleluya!

Iliyotangulia: 119 Mungu Yuko Kati Yetu

Inayofuata: 121 Kulipiza Upendo wa Mungu na Kuwa Shahidi Wake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki