339 Wewe ni Mwaminifu kwa Nani?

1 Kama sasa Ningeweka utajiri mbele yenu na kuwaambia kuwa mchague kwa uhuru, huku Nikijua kwamba sitawahukumu, basi wengi wangechagua utajiri na kuacha ukweli. Wazuri miongoni mwenu wangeacha utajiri na kuchagua ukweli shingo upande, ilhali wale ambao wako katikati wangekumbatia utajiri kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine kuukumbatia ukweli. Kwa njia hii, je, rangi zenu halisi si zingejidhihirisha? Unapochagua ukweli kwa kulinganisha na kitu chochote ambacho u mwaminifu kwacho, wote mtafanya maamuzi kama hayo, na tabia yenu itabakia kuwa ile ile. Je, hakuna watu wengi miongoni mwenu waliobadilika badilika katika kuchagua baina ya wema na ubaya? Katika mashindano kati ya mazuri na mabaya, nyeusi na nyeupe, mna uhakika na uchaguzi mlioufanya kati ya familia na Mungu, watoto na Mungu, amani na vurugu, utajiri na umasikini, hadhi na kuwa mtu wa kawaida, kusaidiwa na kutupiliwa mbali, na kadhalika.

2 Kati ya familia yenye amani na familia iliyovunjika, nyinyi huchagua ya kwanza bila kusita; kati ya utajiri na wajibu, safari hii pia mnachagua ya kwanza, bila kuwa na nia ya kurudi ufuoni kati ya starehe na umasikini, tena mlichagua ya kwanza; kati ya watoto, mke, mume na Mimi, mnachagua za kwanza; na kati ya dhana na ukweli, kwa mara nyingine tena mlichagua ya kwanza. Nikikabiliwa na kila namna ya matendo yenu maovu, karibu sana Nimepoteza imani Yangu kwenu. Ninashangazwa sana na kwamba mioyo yenu inapinga kulainishwa.

3 Miaka mingi ya kujitolea na jitihada Yangu imeniletea kuvunjika moyo tu nanyi kupoteza imani Nami. Hata hivyo, matumaini Yangu juu yenu yanakua kila siku inayopita, kwa kuwa siku Yangu tayari imekwisha kuwekwa wazi kwa kila mtu. Lakini, bado mnaendelea kuyafuata yale ambayo ni ya giza na maovu, na mnakataa kulegeza mshiko wenu. Kwa kufanya hivyo, mtapata matokeo gani? Mmewahi kutafakari kwa makini kuhusu hili? Kama mngetakiwa kuchagua tena, msimamo wenu ungekuwa upi? Bado lingekuwa ni chaguo la kwanza? Je, yale ambayo mngenipatia bado yangekuwa maudhi na huzuni ya majuto? Je, mioyo yenu bado ingekuwa migumu? Je bado mngekuwa hamjui cha kufanya ili kuufariji moyo Wangu?

Umetoholewa kutoka katika “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 338 Yako Wapi Maonyesho Yako ya Uaminifu kwa Mungu?

Inayofuata: 340 Kazi Afanyayo Mungu Kwako ni ya Thamani Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp