309 Una Imani na Upendo wa Kweli kwa Kristo?

1 Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kuwa walengwa wa fadhili Zake machoni Pake. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hujitahidi kupata mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii hasa, wengi kati yenu wanajaribu daima kujipendekeza kwa Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe.

2 Kwa nje, nyote mnaonekana kuwa watiifu sana kwa huyu Kristo aliye duniani, lakini kwa kiini hamna imani Kwake wala kumpenda. Ninachomaanisha ni kwamba yule mliye na imani kwake kwa kweli ni yule Mungu asiye dhahiri katika hisia zenu, na yule kweli mnayempenda ni Mungu mnayemtamani usiku na mchana, lakini bado hamjamwona kamwe kibinafsi. Na kuhusu huyu Kristo, imani yenu ni sehemu tu, na upendo wenu Kwake si kitu.

3 Imani inamaanisha imani na kusadiki; upendo unamaanisha kusujudu na kusifu ndani ya mioyo yenu, bila kuondoka. Lakini imani yenu na upendo wenu kwa Kristo wa siku ya leo vimepunguka chini ya hili. Ikujapo kwa imani, mna imani Kwake jinsi gani? Ikujapo kwa upendo, mnampenda jinsi gani? Hamjui kabisa kuhusu tabia Yake, sembuse kiini Chake, hivyo ni jinsi gani kwamba mna imani Kwake? Uko wapi uhalisi wa imani yenu Kwake? Mnampenda jinsi gani? Uko wapi uhalisi wa upendo wenu Kwake?

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 308 Iko Wapi Imani Yako ya Kweli?

Inayofuata: 310 Una Vipengele Vingi vya Kutomwamini Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp